Friday, July 4, 2008

Muziki wa injili Tanzania

Anaitwa Pastor Wambura.Wengi tumezoea kumwona channel 5 katika video yake inayoonyeshwa katika kipindi cha nyimbo za kusifu na kuabudu asubuhi kila siku katika television hiyo.Kumekuwepo na maoni mengi kutoka kwa watu mbalimbali waliofanikiwa kuiona video ya wimbo huo wa pastor wambura inayokwenda kwa jina la "Bwana ndiye Bwana".Wengi wameonekana kuunga mkono style ya uimbaji wa mtumishi huyu anayoitumia ya mtindo wa sebene kama unavyojulikana na watu wengi hapa nchini.Wengine wameonekana kuipinga aina hiyo ya muziki huku wakitoa sababu kuwa muziki huo haumpi Mungu utukufu.Wengine wamefikia hatua huwa wanabadirisha channel wakiona video ya mtumishi huyu inapigwa.
Swali la kujiuliza hapa ni Je,ni muziki upi hasa unaokubalika kibiblia?Je ni bolingo,sebene,reggae,zouku,blues,chacha,charanga,funky,hip-hop,country,rock-n-roll,rhumba,jazz,pop,bongo fleva, na aina nyingine nyiiiiiiingi za muziki unazozijua wewe.Swala hili limekuwa likitutatiza wengi wetu hasa pale tunapohudhuria matamasha ya muziki wa injili na kukutana na mambo haya.

Flora Mbasha mwimbaji wa Injili

Picha kwa hisani ya Strictly Gospel

6 comments:

Anonymous said...

Unajua nyimbo nyingi za dini, sehemu nyingi huimbwa kulingana na tamaduni za watu wa mahali hapo.

Kwa mfano ukienda kongo -ndombolo iko makanisani maana niutamaduni wao.Ukienda Jamaica Reggae iko makanisani maana ni utamaduni wao, halo kadhalika nimeona hata waamerica weusi hiphop ipo sana makanisani kwani ni utamaduni wao.

Ikienda india, arabuni, china, israel kwenyewe na sehemu nying makanisani wanaimba nyimbo za miziki ya kwao.

Kwa kifupi ukisema reggae sebene ni dhambi, ni maana yake hata hao watu wanaoimba nyimbo hizo nchini mwao pia ni dhambi.

Nyimbo za maadhi ya taratibu-blues sio utamaduni wa watanzania japo wengi wanazikubali kutokana na zilivyo.

Sasa je biblie insemaje?? zaburi 150. inasema tumsifu kwa kila kitu, biblia haijasema staili gani inafaaau haifai.Ukitunga wimbo kwa lengo la kumtukuza Mungu, aidha umetumia akili au Roho HAMNA TATIZO.

Hata ikiwa na lengo la kupata hela, shauri yako ili mrradi huo wimbo unanibariki nitaimba,tukihukumu namna hii, hata nyimbo nyingi zinazoimbwa sasa sio tamaduni zetu.

Tamadubi zetu ni ngima za asili na muziki wa dansi!!!! sio taarabu wala zinginezo.

Kwa hiyo Tanzania sasa iko kwenye kipindi cha kuingiliwa na tamaduni za nchi zingine, maana hata hivyo tuko mbioni kupoteza utamaduni wetu.Kongo Afrika kusini nyimbo zao wanazipromoti sana na tunaiga , wka sababu tunaona pengine nyibo zetu mbaya lakini sivyo. tumekosa wataalamu wa kutunza tamaduni.

Nigeria kwa mfana ala za miziki yao ni za nchi yao no matter ameimba kiingereza au kikabila!!!

Kwa upeop wangu huu naona , wimbo wowote unafaa ilimradi unamtukuza Mungu.

Inatatiza pale unapoona sataili ya wimbo wa kilabuni ndio nayo inatu,ika kanisani, lakini UTAMADUNI WETU UKO WAPI MPAKA TULALAMIKE??

Kalenge

Anonymous said...

Duh! uchezaji wa siku hizi hauna heshima hata kidogo, kwa kweli haumpi Mungu utukufu, watu wengi hufanya hivyo kujipatia umaarufu hasa kwa wale wasiookoka! kwa sababu style zimeendana na nyimbo zao, ndo maana nyimbo zao utazikuta bar mtu anakunywa beer lakini huburudishwa na wimbo wa Injili, hakuna Hofu, tunataka mtu akisikiliza wimbo wa INJILI, pale pale dhamira inamshitaki aache njia yake mbaya. Kweli huu uimbaji wa siku hizi ni DILI watu wanaimbaimba tu ili wawavute watu sio Mungu! ndo maana kila siku nyimbo zinabadilika badilika akiimba hivi leo katika UWEPO WA MUNGU kesho amepotea njia kabisa anajiimbia yeye sio kwa UTUKUFU WA MUNGU, kwa maslahi yake kuwafurahisha wasikilizaji wake.

Imani martini said...

Mary dada, unachosema ni sahihi, lakini mara nyingi sio practical.Kwangu mimi ikifikia muda fulani nyimbo za walokole zikaimbwa vilabuni ili kuziondoa nyimbo za wamataifa, kwangu mimi naona ushindi.Je kipindi kile cha miaka ya 60,70 na 80 je ni kila wimbo watu walikuwa wanasikiliza wanachomwa dhamira zao hapohapo??

tumekazana kulalamika bila kujua chanzo ni nini?? wimbo wowote ule hata kama mwimbaji alikuwa rohoni,lakini kuna nafasi ya msikilizaji je anausikiliza wimbo u la??

Wimbo wa mwaitega mtanitambuaje je ni wa kiroho maana unaimbwa mpaka vilabuni na mpaka ze comedy wanaigiza, lakini ukiangalia maneno yake yanachoma.

MUNGU ANATUMIKIWA KWA ROHO NA KWA AKILI PIA.

JE NI NANI YUKO RADHI KUPOTEZA MUDA WAKE MIEZI SITA NA ATOE MKANDA ASIUZE?? AU AKAUZA ASICHUKUE HELA??

JE NI NANI YUKO RADHI KUSEMA TUTOE HELA ZETU KUSAIDIA KWAYA FULANI??

TATIZO SIO WAIMBAJI, TATIZO NI WANAOWACHUNGA HAO WAIMBAJI.

TUNATAKIWA KUIMBA BILA KUJALI PESA, LAKINI PESA ZISITUZUIE ILI KUIMBA.

KUSEMA WAIMBAJI WENGI WANATAKA PESA SI KWELI. NI SAHIHI KUSEAM WAIMBAJI WENGI HAWAJAOKOKA.

MAANA KAMA ROHO AMEKUAMBIA IMBA, IMBA

SISI TUNAOHUKUMU HATUJUI NINI KINAENDELEA NDANI YA HUYO MTU.

KUNA MTU KANDA YA KWANZA INAWEZA IKAPENDWA LAKINI YA PILI HAIJAPENDWA HAIMAANISHI KUWA HAKUIMBA KWA ROHO!!!!! KIPIMO NI NINI?? KANDA KUPENDWA??

MNAWEZA MKAMWITA MPAGANI AKAWAIMBIA WIMBO MZURI NA NYIE MKANENA KWA LUGHA!!!! HAIWEZEKANI??? LAKINI ALIYEIMBA NI MPAGANI AU MWISLAMU KISA ANASAUTI NZURI AU ALA ZA MUZIKI AMEZIPANGILIA.

TUNAWAONEA SANA TUNAPOSEMA WANAIMBA KUPATA FEDHA.
AFADHALI WAIMBAJI KULIKO WACHUNGAJI WENGI WANAOITENGENEZA MIUJIZA ILI WAPATE HELA , HAO NDIO WABAYA ZAIDI.

HITIMISHO NI KUWA WATU WAONGOZWE KWA ROHO NA NENO LA MUNGU KATIKA KILA WAFANYACHO HII NI KAZI YA WACHUNGAJI.WAIMBAJI NI MATUNDA YA KUCHUNGWA KWA HIYO KAMA KUNA LAWAMA YOYOTE ILE WACHUNGAJI WA KULAUMIWA.

LA KAMA HAMNA BADO HATUNA KIPIMO KUSEMA FULANI KAIMBA KWA ROHO NA FULANI HAJAIMBA KWA ROHO, MAANA WASIKILIZAJI NAO WANA NAFASI YAO.

Anonymous said...

Ubarikiwe sana kaka imani kwa maelezo yako mazuri na ya kujenga, suala la kusema tatizo sio la waimbaji bali ni la wanaowachunga ni kweli lakini mimi naona waimbaji wengi hujichunga wenyewe! wanaanza vyema wakiwa na wachungaji wao lakini baadae huishia katika mwili hawawasikilizi wachungaji wao tena, pindi wanapofanikiwa, wapo na WANAFAHAMIKA wakiwaonywa wao hujisimamia wenyewe. Ndio maana hawafiki mbali. NI WAIMBAJI WACHACHE WANAOONGOZWA NA WACHUNGAJI WAO!

Huwezi amini kaka, waimbaji hawahawa unaoona wameokoka au wanaosema wameokoka wachache hawajali pesa wanafanya kazi ya Mungu kwa uaminifu, wengine pesa kwanza na wanakupangia dau ndio waimbe na ukiangalia maisha yao wanajali starehe na mizaha hii SIO SAHIHI, ndio ROHO KASEMA IMBA; IMBA lakini kwa Utukufu WAKE.

Watumishi ni WATUMISHI tu wawe wachungaji ama waimbaji wote wanamtumikia Mungu sasa kuna wale walioitwa katika kazi ya Mungu na wengine wamejiita! wanatumia jina la YESU kwa maslahi yao binafsi, Hii SI SAHIHI, lazima hawatafika mbali.

Huwezi kumlinganisha muimbaji aliyeokoka na ambaye hajaokoka wakawa sawa! hata kama ataigiza vipi, lazima kutakua na tofauti tu! hata kama wote wana sauti nzuri ya namna gani. Kitu hapa ni USAFI WA MOYO; Je moyo UKO SALAMA? na UIMBAJI HUO UNAMTUKUZA MUNGU?

-AHSANTE

Anonymous said...

Ameni dada nimekuelewa kwa upande huo.Kuwa wengi wao wanaamua tu kwenda studio na hawana wachungaji.Na TV ndio hizo zinawapromote.Kumbuka kwa mfano huyu kijana ni mtoto wa mchungaji.N wengi wanakimbia makanisani wanatokea makanisani pale anapojiona anaweza kutoa SINGLE.

TUNA KAZI YA KUOMBA dada yangu.

ubarikiwe

Kalenge

Anonymous said...

Kweli kaka, tunayo kazi ya kuomba. Kwanza tuanze YERUSALEMU!