Tuesday, July 22, 2008

JE! WAFAHAMU KWAMBA WAISRAELI WAISHIO MAREKANI NI KARIBU SAWA NA WALIOKO ISRAEL KWENYEWE?

Kulingana na takwimu zilizotolewa mwaka huu na idara ya takwimu ya Israel (Central Bureau of statistics-CBS), kwenye sherehe za kutimiza miaka sitini ya uhuru wa nchi hiyo,Israel ina jumla ya watu 7,282,000. Kati ya hao 5,499,000 (75.5%) ni Wayahudi, 1,461,000 (20.1%) waarabu na 322,000 (4.4%) wengineo.

Pamoja na idadi hiyo, taifa hili ambalo lilianzishwa na watu kiasi cha 806,000 mwaka 1948 kwa sasa limekuwa kwa kiasi kikubwa na ni taifa ambalo historia yake na habari zinasomwa na kusikika karibu duniani kote kila siku.

Pamoja na kuwa na idadi hiyo ndani ya nchi ijulikanayo kama Israel bado wengi wa wayahudi wanaishi nje ya nchi hiyo. Marekani ni nchi inayoongoza kwa kuwa na wayahudi wengi kwa karibu sawa na wale walio ndani ya Israel kwenyewe. Kama takwimu zinavyoonesha: Marekani 5,275,000 (40.3% ya wayahudi wote duniani), Ufaransa 491,500 (3.8%), Canada 373,500 (2.9%) na nchi nyinginezo nyingi. Kwa takwimu hizo inaonesha kwamba bado wayahudi wengi wanaishi katika utawanyiko.

Wataalamu wa maandiko katika hili mnasemaje? Je kuja kwa Kristo ni mpaka Israeli wote warejee kwao au ishara kubwa ni ile ya habari njema kuhubiriwa ulimwenguni pote kama inenavyo mathayo 24 na sura nyinginezo za kinabii au?

No comments: