Monday, July 7, 2008

FURAHIA WOKOVU WAKO (ENJOY YOUR SALVATION)

MUNGU ASIFIWE SANA!
Pamoja na kuurithi uzima wa milele,kuna ahadi nyingi sana ambazo Mungu amewaahidi wale wamchao yeye,yaani waliokoka,kwahiyo ni jukumu letu sisi kumuuliza Mungu ili azitimize ahadi zake.
Kuna watu wengi sana ambao wameokoka kweli lakini wanaishi maisha duni,ya kimasikini kabisana ya kinyonge kabisa,ukiwauliza wanafikiri kuwa wameokoka ili tuu wasiende Jehanamu,kwahiyo hawahitaji kuishi maisha mazuri hapa duniani.Jambo hilo si kweli na wanamsingizia Mungu wetu tuu.Ukweli Mungu anataka mtu aliyeokoka afaidi maisha yote ya hapa duniani pamoja na yale yajayo.Mungu hataki mtu wakeasumbuliwe na umasikini,magonjwa,kuonewa kwa namna yeyote ile,kudharauliwa kufeli au hali yoyote mbaya maana hebu jiulize mtu wa Mungu,kuna faida gani basi kuokoka kama mtu utaendelea kuonewa na shetani?Ukweli ni kwamba mtu akishaokoka anakaa ndani ya Yesu na Yesu anakaa ndani yake,na ufahamu kuwa Yesu si masikini bali ni tajiri,na akiaa mahali,umasikini hauna nafasi,Yesu si mgonjwa bali ni Daktari bingwahivyo magonjwahayakai sehemu alipo Yesu.Ndio maana wakimbizi hukimbia kutoka kwenye nchi zenye vita nakwendakwenye nchi zenye amani na utulivu kuliko za kwao.
Ingekuwa nia ya kokoka ni kwenda mbinguni tuu,basi Yesu asingeponya watu,kutoa pepo,kubariki wala asingetupa karama za uponyaji kutoka kwa MUNGU.
Hebu tujifunze namna ya kufurahia maisha ya wokovu baada ya kuokoka.
BAADA YA KUOKOKA:
1. Watu wengi wamakuwa hawamini ya kuwa Mungu amewasamehe dhambi zao zote pale wanapokoka,jambo hili limekuwa likiwarudisha wengi nyuma.Unapookoka amini kuwa umeokoka na kwamba Mungu baba amekusamehe dhambi zako zote na kuzisahau kabisa tena zote kabisa,haijalishi ni dhambi ya namna gani uliwahi kuifanya,Mungu anasamehe na kuzisahau kabisa.Soma ISAYA43:25,ISAYA 1:18,ISAYA 44:22.
2. Kuwa na ushirika na watu wengine ambao watakujendakiroho,kama vile vikundi vya maombi na vile vya uamsho.SomaWAEBRANIA10:25,MATENDO YA MITUME 2:42.
3. Hakikisha kuwa unasoma na kutafakari neno la Mungu katika Biblia kila siku,mara nyingi iwezekanavyo,neno la Mungu litakupa mwongozo wa namna ya kuenenda katika wokovu,pia litakufundisha namna ya kuufurahia wokovu wako,hebu soma1PETRO2:2,WAEBRANIA 4:12,ZABURI 119:7&41&43.
4. Dumu kwenye maombi mara zote ukimueleza Mungu mahitaji yako yote kwakuamini kuwa anakusikia na atakupa yale yote unayomuomba.
5. Fahamu kuwa sasa umekuwa mtoto wa Mungu na kwa hiyo Mungu ndiye baba yako(YOHANA1:12),WARUMI8:16)
6. Mkimbie shetani na kazi zake zote,na tamaa zake zote kwa ujasiri(ZABURI 1:1)
7. Usisite kuwafahamisha wengine juu ya uamuzi wako wa kuokoka,watu wengi wamekuwa waoga wa kukiri mbele za watu kuwa wameokoka ,hilo ni jambo la hatari sana katika maisha ya kiroho.Wote waliokoka ni ndugu ndani ya Kristo.Je,wewe hupendi kufahamiana na ndugu zako??Yesu akusadie ili uweze kumkiri mbele ya watu wote.
8. Sasa fuata maagizo yote ambayo Mungu amekupa kwenye neno lake(BIBLIA) ISAYA 44:22.
MKUMBUSHE MUNGU AHADI ZAKE:
Ikiwa umeamua kumfuata Mungu,yeye anakusikiliza kama mtoto wake,kumbuka Biblia inasema"wote waliompokea aliwapa uwezo kuwa wana…"(YOHANA1:12)Kwa hiyo sasa zungumza na Mungu katika maombi ukimkumbusha ahadi zake ambazo amesisema katika Biblia.Ukishaokoka Mungu anakuwa karibu na wewe kuliko baba yako wa duniani alivyokaribu na wewe. Liamnini jina la Yesu.1PETRO2:3-5,MARKO 16:17-18,1WAKORINTHO3:16-17.
MAOMBI:Narudia tena ya kuwa ni muhimu sana kuzungumza na Mungu kwa maombi mara kwa mara kila siku.Hebu soma mistari ifuatayo,ISAYA43:26.".njoo tuhojiane,nikumbushe shida zako,eleza shida zako upate kupewa haki yako…",YEREMIA29:12.
Mtu waMungu unayefuatilia somo hili kumbuka siku zote kwambamaombi bila neno ni sawa na ndege aliyevunjika bawa moja .Sikuzote Mungu huwa hajibu maombi bali huwa anajibu neno lake ambalo limo huko ndani ya maombi yako wewe muombaji,tazamaYEREMIA 1:12,Kwa hiyo,
Siku zote ingiakwenye Maombi ukiwa na neno la Mungu(mstari au mistari ya Biblia inayoelezea ahadi ya Mungu juu ya lile unaloomba k wake) Unapomuomba Mungu usiangalie majibu yako kwa jinsi ya kimwili,wewe unachotakiwa kufanya ni kuamini tuu kuwa umeshapewa.Ukisoma kitabu cha 1WAFALME 18,utaona namna ambavyo Eliya aliomba kwa Mungu ili mvua inyeshe juu ya ile nchi.Nabii Eliya aliomba akamtuma mtumishi wake kwenda kutazama kama kuna dalili zozote za mvua(mawingu)lakini hazikuwepo,akandelea kuombakwa juhudi,Hebu sema"akaendelea kuomba kwa juhudi"akafanya hivyo mara saba na ile mara ya saba akaona mawingu angani madogo kiasi cha kiganja cha mkono.Nabii Eliya alipoona ishara hiyo ndogo aliamini kuwa mvua itanyesha na akafurahi sana kwa kuwa Mungu amejibu maombi yake.Hata wewe unayesoma somo hili sasa hivi uwe na tabia kama ya Eliya.Kama bado hujaona ishara yoyote ile,endelea KUOMBA KWA JUHUDI.Ukiona ishara kidogo sana,ANZA KUMSHUKURU MUNGU UKIAMINI KUWA AMESHAKUJIBU OMBI LAKO.BWANA YESU ASIFIWE SANA!!!! Na baada ya muda mfupi sana utayaona majibu yako waziwazi kabisa.HALELUYA!!
AHADI ZA MUNGU:Ndugu yangu katika Kristo Yesu,hapa nitakupa kwa kifupi tuu baadhi ya ahadi ambazo Mungu amezisema kwa ajili yangu na yako.Ahadi za Mungu zinapatikana katika Biblia.Nakushauri usome Biblia zaidi ili uweze kufahamu ahadi nyingine kwa maana zipo nyingi SANA.
Ahadi hizo nimeziandika katika website yangu www.lema.or.tz click hapa kuzisoma. Kumbuka kuwa mwananchi asipofahamu haki zake, hataweza kuzidai, hali kadhalika mtu aliyeokoka (mlokole) asipozifahamu haki zake, hawezi kuzidai kwa Mungu. Ninakushauri usome Neno la Mungu kwa bidii KILA SIKU ili uone ahadi ambazo Mungu amekuwekea na uanze kuziomba kwa Mungu.
Imetosha sasa watu kuwadharau walokole.

Naamini utalisoma hili somo kwa wiki hii nzima na litakusaidia sana.Waalike na wengine kujiunga na mailing lists hii.
Tafadhali endelea kuniombea.

Mungu akubariki sana.
Frank Lema,
Arusha

No comments: