Wednesday, July 30, 2008

Ushuhuda..Ushuhuda...Ushuhuda...!

Kama nilivyowaahidi watumishi kuwa tutakuwa tunawaletea mbalimbali za matendo makuu ya Mungu anayotenda kwetu sisi watumwa wake..
Wapendwa,
Bwana YESU asifiwe sana!!!! Jina langu ninaitwa Prudence, nimeona ni vema ku share ushuhuda huu wa matendo makuu ya MUNGU kwangu na kwa familia yangu kwa ujumla. Sisi sote ni shuhuda wa matendo makuu ambayo MUNGU hututendea kila kuitwapo leo, pumzi ya uhai, afya njema, chakula na baraka nyingine nyingi. Mimi nimemwona MUNGU zaidi ya hapo. Mwaka 2006 tarehe 12 mwezi Februari, gari letu aina ya Suzuki ESCUDO 5 doors, iligongwa vibaya sana na FUSO hapo Morogoro maeneo ya Mkambarani karibu na Mikese Polixce station.
Ninawaambia wapendwa gari lile liligongwa vibaya sana upande ule wa dereva, nilishuhudia kwa macho yangu ya nyama jinsi dereva alivyo vyunjwavyunjwa miguu na maeneo mengi ya mwili wake. Aliumizwa kichwa na kwa hakika aliumia sana, kiasi kwamba hakuweza kuishi zaidi ya saa moja tangu tupate ajali. Kijana MOSES, ambaye alikuwa dereva, alifariki DUNIA katika hospital ya MOROGORO. Inaniuma sana.
Kwa upande wangu mimi, nilivunjika mkono wa kulia na mikwaruzo michache sehemu za tumboni. Sikuumia sehemu nyingine yoyote na mkono hauna madhara tena ninautumia kama kawaida na huwezi jua kama uliwahi kuvunjika. Wapendwa hebu angalieni wenyewe hizo picha halafu mniambie kama si MUNGU aliye niokoa ni nani hasa??? Nina mshangaa MUNGU, nina muogopa na ninamheshimu. MUNGU anaweza yote, hata pale unapoona imeshindikana kwa akili za kibinadamu yeye bado anaweza.!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mimi na familia yangu tumemwona BWANA YESU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
shuhuda
Kama unao ushuhuda na unapenda kushirikisha wapendwa wengine mahali hapa katika mlima huu wa sayuni , usisite kuniandikia kwa email: miwlc@yahoo.com

3 comments:

Maranatha said...

Duuuuhhh!! Aieehh!! Kweli Ashukuriwe Mungu! Kama ndugu ulitoka humo ndani salama, basi jina la Bwana libarikiwe na mwacheni Mungu aitwe MUNGU! Moyo wangu wamtukuza Bwana pamoja nawe!

Amina

savedlema said...

Mh,Bwana Apewe sifa!
Kwa kweli ndugu zangu Yesu ndiyo mwenye nguvu na upendo mkuu,nafikiri hiyo inaingia kwenye C.V yake, hiyo ya kumwokoa huyu mama.
We are all safe, we who depend on Christ.

Anonymous said...

Uhai wetu, sisi tulio ndani ya Yesu unavuka mipaka ya mwili huu. Kuishi ni Kristo na kufa ni faida. Tukiwa ndani ya Yesu tu salama, si kwa sababu tunaishi matika mwili huu bali kwa sababu tunaishi milele. Kifo cha mwili huu ni geti la kungia furaha ya Milele! Watakatifu wengi wanakufa kwenye ajali, si kwa sababu Mungu ameshindwa kuwaokowa na ajali hizo. Lakini mtakatifu akisalimika na akaendelea kuishi ajuwe ana kazi kubwa ya kufanya kumtumikia Mungu na kuendelea kuishindania zaidi imani ili siku yake ikifika awe bado ni mtakatifu.

Ndugu, endeleeni kumtumikia Bwana Mungu!