Mathayo 10:8 "Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure."
Angalia kwa makini video hii utaona jinsi mama huyo wa huko Nigeria aliyoamua kung'ang'ania ahadi za Bwana na hata akamlilia Mungu na kuchukua hatua ya imani kuubeba mwili wa mume wake aliyekuwa amekufa na kuupeleka kwenye mkutano kanisani ambapo Mwingilisti Bonke alikuwa anaombea watu...
Fuatilia series hii utaona jinsi Mungu wetu tunayemuamini alivyo wa rehema na upendo na uwezo mwingi zaidi ya kufufua maiti na kuleta uhai wa mwili lakini anaweza kuleta uhai wa roho yako ili isiangamie milele katika moto wa jehanamu...
angalia ushuhuda huu sehemu ya 1.
Sehemu ya 2
Sehemu ya 3
"Jesus has finished the mansions but the saints are not ready.."
Sehemu ya 4
Sehemu ya 5
Sehemu ya 6
YESU KRISTO anaweza yote.Ushuhuda mkubwa zaidi ya yote ni wewe kumpa YESU maisha yako awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.Biblia inasema itamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote na baadaye kuukosa ufalme wa mbinguni..?
Kama unataka kumpa YESU maisha yako, omba maombi haya mafupi na utaokoka.
"Bwana YESU.
Mimi ni mwenye dhambi.
Natubu dhambi zangu zote nilizozitenda.
Naomba unisamehe na unitakase kwa damu yako iliyomwagika msalabani kwa ajili ya wokovu wangu.
Nakukiri kwa kinywa changu kuwa wewe ni Bwana na mwokozi wa maisha yangu.
Futa jina langu katika kitabu cha hukumu ya milele na moto wa jehenamu.
Andika jina langu katika kitabu cha uzima wa milele.
Nipe roho wako mtakatifu na uniwezeshe kuishinda dhambi.
Kwa jina lako YESU KRISTO mwana wa Mungu aliye hai naomba.
Amen."
Kama umeomba sala hii fupi.Tuandikie kwa email hizi hapa chini ili tuombe pamoja na wewe ili uweze kukua katika wokovu.
miwlc@yahoo.com
savedlema2@yahoo.com
No comments:
Post a Comment