Azma ya Tanzania kutaka kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC), imezidi kupata nguvu, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwataka Watanzania waondokane na woga wa kuiogopa jumuiya hiyo. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Membe alipozungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya wizara hiyo, jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku moja baada ya Naibu wake, Balozi Seif Ali Iddi, kukaririwa na gazeti hili jana akiweka bayana kuhusu azma hiyo. Alisema anawashangaa baadhi ya Watanzania kutoa kauli zinazoashiria kuiogopa OIC na baadhi ya nchi za Kiislamu, kama vile Iran, wakati wanasifika kuwa ni watu jeuri na majasiri wanaoweza kumudu kukabiliana na mambo makubwa, mazito na ya kutisha. Membe alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa wanahabari, ambaye katika maelezo yake, alionyesha wasiwasi kuhusu msimamo wa serikali kuwa na uhusiano na Iran na azma yake ya kutaka kujiunga na OIC. Mwandishi huyo alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, moja ya nchi za Kiislamu iliwahi kuingiza nchini msaada wa mchele, huku vifurushi vyake vikiwa vimewekwa juu yake misahafu ya Kur�ani Tukufu kwa nia ya kuwasilimisha Watanzania. Leo pia, katika utawala wa Rais Muislamu tunaelezwa kuwa Tanzania inataka kujiunga na OIC, kitu ambacho mimi nitakipinga hadi dakika ya mwisho,� alisema mwanahabari huyo. Wasiwasi wa mwanahabari huyo ulikuja baada ya Membe kueleza hatua nzuri iliyofikiwa katika mazungumzo kati yake na Rais wa Iran, Mahmoud Ahmednejad ambayo yalilenga kuiomba nchi hiyo kufuta madeni inayoyadai Tanzania yapatayo zaidi ya Sh bilioni 200. Membe aliitisha mkutano huo kwa lengo la kuipongeza nchi ya Uganda kwa kuwa mwanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kusema kuwa kuingia kwa nchi hiyo kutasaidia katika utatuzi wa migogoro inayolikumba Bara la Afika. Kauli ya mwandishi huyo, ilimfanya Waziri Membe ambaye awali katika mkutano huo na waandishi wa habari alizungumza kwa upole, umahiri na kwa ufasaha wa hali ya juu, abadilike na kuanza kuzungumza kwa ukali. Kwa nini tunashikwa na uoga? Tukipewa msaada na Marekani tunaambiwa kuna mkono wa mtu, tukipewa na Iran tunaambiwa hivyo. Niambieni mimi kama Waziri wa Mambo ya Nje niende wapi?, alihoji Membe na kumtaka mwandishi huyo amtajie japo nchi mbili duniani ambazo ni takatifu kwa asilimia mia moja ili Tanzania ijenge uhusiano nazo na iachane na nchi nyingine. Alisema kwa mfano Uganda, ambayo ni mwanachama wa OIC, asilimia 66 ya wananchi wake ni Wakristo, asilimia 10 tu ndio Waislamu na asilimia iliyosalia ni ya watu wasio wa dini hizo na pia, mapapa watatu wamewahi kwenda nchini humo. Hata hivyo, Membe alisema pamoja na Uganda kujiunga na OIC, idadi ya Waislamu wala misikiti haijaongezeka nchini humo. Kutokana na hali hiyo, alisema haoni ubaya mtu kunufaika na fedha za shetani na kwamba, kitendo cha Watanzania kuiogopa jumuiya hiyo na Iran, ni kujivua sifa yao ya ujeuri na ujasiri na pia ni kushindwa kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye hakuwa anaogopa hata kitu kimoja. Kama unakuta shetani mahali ana hela si uchukue. Ujeuri wetu uko wapi? Kwa nini tunaiogopa Iran. Ukiona mchele umewekwa Kur`ani, hiyo Kur`ani si unaitupa tu, halafu unakula mchele?`` alisema Membe. Hata hivyo, Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake katika miaka ya 1990 aliwahi kukemea hatua ya Zanzibar kujiunga na OIC kwa kuwa ilikuwa ni ukiukaji wa katiba, licha ya maelezo kwamba ingevinufaisha visiwa hivyo kiuchumi. Katika makemeo yake, Mwalimu Nyerere alisema hawezi kukaa kimya kuruhusu Zanzibar inufaike kwa kuvunja Katiba ya nchi. Hata hivyo, Waziri Membe jana alisema suala la Tanzania kujiunga na OIC au la, litaamuliwa na wananchi wenyewe na kusisitiza kuwa aliposema bungeni Agosti 22, mwaka huu kwamba, kujiunga na OIC hakuna madhara hakumaanisha kuwa Tanzania imeshajiunga na jumuiya hiyo. ``Tuiache Israeli iiogope Iran. Tuna ubalozi wa Iran, hatukuwafukuza. Kwa nini tunaogopa na jeuri zetu. Uamuzi huu utafanywa na Watanzania wote, serikali kazi yake ni kutoa changamoto. Naomba Watanzania tujiamini. Hata Tanzania tunachukiwa kwa kuishambulia Uganda, lakini tulikuwa na sababu. Kama (serikali) tungekuwa na woga tusingejiunga na Marekani kwa sababu hawa (Marekani na Iran) ni maadui`` alisema Membe. Jana gazeti hili lilimkariri Balozi Iddi akisema kwamba mchakato kwa Tanzania kujiunga na OIC unatarajiwa kuanza wakati wowote na kwamba, hatua ya mwanzo ya mchakato huo. Alisema viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano watakutana na wenzao wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa ajili ya kupata msimamo wa pamoja kuhusu suala hilo. Naibu Waziri huyo alisema hayo alipoulizwa na Nipashe kama mchakato kwa Tanzania kujiunga na jumuiya hiyo umeshaanza au la tangu Waziri Membe atoe kauli hiyo bungeni, mjini Dodoma, Agosti 22, mwaka huu. Alisema mchakato kwa Tanzania kujiunga na OIC ni mrefu, ambao unatarajiwa pia kulishirikisha Baraza la Mawaziri kufikia maamuzi. Balozi Iddi alisema hatua nyingine ya mchakato, ambayo serikali inatarajia kuichukua, ni kutoa elimu kwa umma ili kuwaondoa uoga wote walioonyesha hofu iwapo Tanzania itajiunga na jumuiya hiyo. Agosti 22, mwaka huu Waziri Membe wakati akifunga mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake, alisema hakuna madhara yoyote kwa Tanzania kujiunga na IOC.
SOURCE: Nipashe
WAPENDWA WANA SAYUNI.SISI KAZI YETU NI KUOMBA TU.LEO TUPO SIKU YA TATU YA MAOMBI YETU.NENO LA KUSIMAMA NALO NI LILE LILE LA 2NYAKATI 7:14.
KAMA UNAPENDA KUUNGANA NA SISI KUHUSU MAOMBI HAYA TUANDIKIE KWENYE EMAIL HII: MIWLC@YAHOO.COM
if my people, who are called by my name, will humble themselves and pray and seek my face and turn from their wicked ways, then will I hear from heaven and will forgive their sin and will heal their land. Now my eyes will be open and my ears attentive to the prayers offered in this place.
No comments:
Post a Comment