Sunday, October 26, 2008

Masheikh kuwajibu Maaskofu kuhusu OIC:MAOMBI MLIMA SAYUNI:TUPO SIKU YA TANO

SUALA la Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislaam (OIC) limechukua sura mpya baada ya masheikh kutoka tasisi na madhehebu mbambali kufanya kikao cha dharura jana na kujipanga kutoa msimamo wao Ijumaa ijayo.
Masheikh hao ambao ni Maimamu wa misikiti mbalimbali jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za kiislaam nchini baada ya mjadala huo walitoka na msimamo kuwa watatangaza uwanja baadaye na kuwajibu maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) waliotoa tamko la kupinga Tanzania kujiunga OIC na kumtaka Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anayelishadadia ajiuzulu.
Katibu wa Kamati ya masheikh hao, Ramdhan Sanze alithibitisha kuwa tamko lao litatolewa Ijumaa.
“Kwa kweli askofu kumwambia waziri apewe kadi nyekundu kwa kukubali jambo lenye maslahi kwa taifa si kauli nzuri na ni kiburi, sasa tunataka kujua kiburi hiki wamekitoa wapi?” alihoji Sheikh Sanze.
Alifafanua kama maaskofu wanatumia kigezo cha katiba ambacho hakina nguvu kwa sababu katiba ipo kwa maslahi ya Watanzania wote wa dini, makabila na rangi zote.
“Kama wao hawataki na hawawezi kukubali Tanzania ijiunge na OIC na sisi pia hatutaki na wala hatuwezi kukubali kukosa manufaa makubwa ya kijamii na kiuchumi kutokana na vikwazo vyao,” alisema Sheikh Sanze.
Sheikh Sanze alisema kuwa kama hali itakuwa hivyo wataona baada ya jahazi kuachana nani atachukua nini.
“Masheikh wamekubaliana kuwa tutoa tamko letu rasmi na zito siku ya Ijumaa ijayo na tena tutalitoa uwanjani, ni uwanja gani na saa ngapi yapo katika mchakato na tutatangaza,” alisema Sheikh Sanze.
Sheikh Sanze alisema watahoji mtazamo na msimamo wa serikali kuhusiana na kiburi cha maaskofu hao wa CCT kujiunga na OIC.
Alisema Tanzania si ya wakristo wala waislaam bali ni ya wote kwa hiyo kila mmoja ana haki ya kupata kile anachostahili kupata bila ya kuwekewa vikwazo na imani nyingine.
Aliongeza kuwa suala la Mahakama ya Kadhi na OIC si mapya kwa Tanzania kwa sababu yalikuwepo na hakuna madhara yoyote waliyoyapata Watanzania kutokana na uwepo wake.
“Hili si jambo jipya lilikuwepo na tulikuwa tunafaidika sana kwa hiyo ni kulirejesha tu na wala si la kuasisiwa upya,” alisema Sheikh Sanze.
Kwa mujibu wa sheikh Sanze OIC ni taasisi inayoongoza kwa kutoa misaada na mikopo yenye riba nafuu duniani kote, hivyo Tanzania ina kila sababu ya kujiunga na Jumuiya hiyo.
“Hapa tatizo si dini tatizo ni kwa kiwango gani Watanzania watafaidika na iwapo nchi yao itakuwa mwanachama wa OIC bila kujali dini,” alisema Sheikh Sanze.
Alisema Tanzania inajiunga na Jumuiya mbalimbali za kimataifa ambazo zinatoa misaada na mikopo kwa nchi yetu yenye masharti magumu na kuhoji kwa nini OIC ipingwe.
Juzi CCT ilitoa tamko la kumwonya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuwa kauli zake kuhusu kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC) zinaweza kusababisha mgawanyiko wa kitaifa na kumtaka aachane nazo au ajiuzulu wadhifa wake.
Tamko hilo la maaskofu wa makanisa ya Kikristo limekuja baada ya Waziri Membe kukaririwa akisema kuwa hakuna athari zozote kwa Tanzania kujiunga na taasisi hiyo, ambayo madhumuni yake ni kutetea binadamu na hasa Waislamu na sehemu takatifu.
Wakitoa tamko lao kwa waandishi wa habari juzi, maaskofu hao kutokana makanisa ya kiprotestanti walisema kauli ya Waziri Membe ina lengo la kutetea maslahi ya watu wachache.
Katika hatua nyingine maaskofu zaidi ya 300 wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, (KLPT) waliokuwa wanakutana jijini Dar es Salaam, nao wamepinga serikali kudhamiria kujiunga na OIC na kuonya kwamba taifa litasambaratika.
Mwangalizi Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Philemon Tibanenason alisema wao kama kanisa wanalipinga hilo kwa kuwa lipo nje ya katiba. “Nchi inakoelekea si pazuri, mfano kutumika kwa uislamu na ukristo, ni kinyume na katiba.
Tayari vikundi vya waumini na taasisi mbalimbali vimekwishatoa misimamo yao kupinga hatua ya Waziri Membe na msaidizi wake, Seif Alli Iddi juu ya suala hilo.
“Dini ni nje ya serikali ndiyo maana hakuna Waziri wa Uislamu…sisi kama kanisa kwanza tunashangazwa na hii ya kupeleka masuala ya dini bungeni, kuzungumza masuala ya dini bungeni, pia ni kinyume na katiba…sisi hatuna dini sasa iweje leo hii tunaingiza mijadala ya kidini?
“Hatuchukii dini wala Uislamu, lakini tunachopinga ni nchi kuendeshwa katika misingi hiyo. Tunaona Pakistan, Sudan, Lebanon, kila kukicha ni mapigano…,” alisema Tibanenason.
Aliongeza kusema: ”Kanisa linapenda kuitahadharisha serikali na kuitaka kusimamia bila woga katiba yetu kwa kuwa serikali imepewa dhamana hiyo na wanachi kwa kiapo.
”Sisi kama kanisa la Pentekoste Tanzania, tunaungana na wote hao kupinga kwa nguvu kusudio hilo la serikali..kazi ya kutangaza, kueneza na kuamini ni suala la mtu binafsi na uendeshaji wa taasisi ni nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
Akisisitiza, Tibanenason alisema kujiunga na OIC kutaleta mgawanyiko na hofu katika jamii huku akiiunganisha na Mahakama ya Kadhi kuwa haina mashiko kwa jamii nyingine isiyo ya Kiislamu.
Alisema kwa kuwa serikali ina chombo chake cha kutoa haki kwa wananchi, kama mahakama, na kuiingiza Mahakama ya Kadhi ni kuinyang’anya serikali mamlaka yake ya utoaji na usimamizi wa haki sawa kwa wananchi wake. Mahakama hiyo haiwezi kukubalika katika taifa ambalo si la Kiislamu
Akizungumzia suala la ufisadi, alisema ni matokeo ya ubinafsi wa viongozi wengi. ”Wengi wamekosa upendo, ni wapenda pesa kiasi cha kusahau maadili ya uongozi. Watu wanaopewa madaraka si waadilifu tena na ingekuwa inawezekana, wangeenguliwa kutoka madarakani ili tutafutwe waadilifu wa kweli.
”Watu wanafahamika, tunadhani hata Rais anatakiwa kuangalia watu waadilifu, tunataka ateue watu wenye moyo wa kweli wa kuipenda nchi na watu wake,” alisema.
Juu ya mauaji ya maalbino, alisema azimio la mkutano wao ulioanza Alhamisi iliyopita hadi jana, ni kwamba serikali iwanyang’anye waganga wa jadi leseni za kuendesha biashara zao kwa kuwa ni chanzo na wachochezi wa mauaji.
Source:Mwananchi


WAPENDWA WANA SAYUNI.SISI KAZI YETU NI KUOMBA TU.LEO TUPO SIKU YA TANO YA MAOMBI YETU.NENO LA KUSIMAMA NALO NI LILE LILE LA 2NYAKATI 7:14.KAMA UNAPENDA KUUNGANA NA SISI KUHUSU MAOMBI HAYA TUANDIKIE KWENYE EMAIL HII: MIWLC@YAHOO.COM


if my people, who are called by my name, will humble themselves and pray and seek my face and turn from their wicked ways, then will I hear from heaven and will forgive their sin and will heal their land. Now my eyes will be open and my ears attentive to the prayers offered in this place.

No comments: