Friday, October 17, 2008

Billy Graham kusherekea Birthday yake ya 90!

BWANA YESU ASIFIWE!
Ndugu wapenzi wa Mlima Sayuni, sina shaka kuwa wengi mnamfahamu au mmewahi kumsikia sana Mtumishi wa Mungu mzee Billy Graham wa USA, namna ambavyo amekuwa akimtumikia Mungu kwa zaidi ya miaka 60 sasa. Mnamfahamu pia mtoto wake anayeendeleza kazi hii ya Injili, aitwaye Franklin Graham. Familia yake ipo kwenye kipindi cha furaha kuu kwani mtumishi huyu wa Mungu (Billy Graham) anasheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa(Birthday) November 7,hii ikiwa ni ya 90!

Mtoto wake na wanatimu wote wa shirika lake la kueneza Injili wamewakaribisha watu wote ambao wamewahi kuguswa na huduma ya mtumishi huyu kushiriki katika sikukuu yake hiyo, kwa njia ya internet. Unaweza kubonyeza (Clicking) hii picha yake na utaletewa mahali utakapoweza kumwandikia Ujumbe mfupi ambao atasomewa katika hiyo sikukuu yake.

Sisi kama watumishi wa Mungu, tunajisikia furaha na amani sana tunapoona Bwana amempa uhai na afya njema hata katika umri huu wa miaka 90! Je, hili nalo siyo moja ya matendo makuu ya Mungu? Hakika! Hii itutue moyo sisi wote tunaomwamini Bwana, Biblia inasema "Tutalala katika umri mwema" ,"tukiwa tumeshiba siku nyingi" tena "Sitakufa bali nitaishi niyatangaze matendo ya Bwana" Tunauona huu kama ushuhuda wa Upendo wa Baba yetu aliye juu.

Je, una lolote la kusema kuhusu hili? tueleze.

Mungu akubariki, nawe "usife bali uishi na kuyatangaza matendo makuu ya Bwana"

Sisi wana-Sayuni wote tunambariki ndugu Billy Graham katika Jina la Yesu na kumwombea miaka mingine MINGI kwa utukufu wa Baba.-Amen.

2 comments:

Anonymous said...

ubarikiwa mtumishi Lema kwa taarifa hizi, nilikuwa sina hii taarifa.

Mtade,

India

Anonymous said...

jina la Bwna libarikiwe,na tuenenze injili ya kristo kwa ushujaa mwingi kama mtumishi huyu,our role model