Sunday, October 26, 2008

Askofu Gamanywa na Askofu Kakobe wamjia juu Waziri Membe kuhusu OIC:MAOMBI YA WANASAYUNI :LEO TUPO SIKU YA 5

Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekosti Tanzania (PCT), Askofu Sylvester Gamanywa, alisema pingamizi la maaskofu dhidi ya Mahakama ya Kadhi na OIC, siyo chuki dhidi ya Uislamu, OIC na mahakama hiyo, bali linalenga kuzuia mgawanyiko wa kitaifa, ambao alisema hautawanufaisha wanaotaka kutekelezewa maslahi yao. Alisema maaskofu wamelazimika kuweka pingamizi hilo kwa vile hawakushirikishwa katika mambo hayo hata katika mazingira ya kawaida na kwamba wamekuwa wakiulizwa na waumini wao makanisani kuhusu mambo hayo. ``Naomba Rais atumie hekima na busara katika jambo hili,`` alisema Askofu Gamanywa.
Askofu Mkuu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship amesema suala la kujiunga na OIC ni la kijinga na hivyo amemtaka Membe na naibu wake wajiuzulu mara moja kwa vile wanataka kuliingiza taifa kwenye machafuko makubwa. Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, kiongozi huyo aliyeonekana kuwa na hasira alisema kama Waziri Membe anataka kusilimu na kupokea fedha, basi asilimu mwenyewe, lakini asiwalazimishe Watanzania. ``Hakuna ujinga unaonikera kuzidi huu wa kujiunga na OIC, Mwalimu Nyerere alisema mtu yoyote anayefikiri kwamba Tanzania inaweza kuwa nchi ya Kiislamu au ya Kikristo ni mjinga, anachokifanya Membe hivi sasa ni ujinga mtupu,`` alisema kiongozi huyo kwa ukali. Akijibu hoja za Waziri Membe na Naibu wake Balozi Seif Iddi walizotoa kwa nyakati tofauti, Askofu Kakobe alisema hapahitajiki utafiti wala zoezi la kuthibitisha ubaya wa kujiunga na OIC kwani jina lenyewe la Jumuiya hiyo linajitambulisha kuwa ni chombo cha Kiislam. Tamko la CCT limetolewa siku moja baada ya Waziri Membe, kukaririwa na gazeti hili jana akiwataka Watanzania waondokane na woga wa kuiogopa OIC. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Membe alipozungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya wizara hiyo, jijini Dar es Salaam juzi, ikiwa ni siku moja baada ya Naibu wake, Balozi Seif Ali Iddi kukaririwa na gazeti hili akiweka bayana kuhusu azma hiyo. Membe alisema anawashangaa baadhi ya Watanzania kutoa kauli zinazoashiria kuiogopa OIC na baadhi ya nchi za Kiislamu, kama vile Iran, wakati wanasifika kuwa ni watu jeuri na majasiri wanaoweza kumudu kukabiliana na mambo makubwa, mazito na ya kutisha. Membe alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa wanahabari, ambaye katika maelezo yake, alionyesha wasiwasi kuhusu msimamo wa serikali kuwa na uhusiano na Iran na azma yake ya kutaka kujiunga na OIC. Kutokana na hali hiyo, Membe alisema haoni ubaya mtu kunufaika na fedha za shetani na kwamba, kitendo cha Watanzania kuiogopa jumuiya hiyo na Iran, ni kujivua sifa yao ya ujeuri na ujasiri na pia ni kushindwa kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye hakuwa anaogopa hata kitu kimoja. ``Kama unakuta shetani mahali ana hela si uchukue. Ujeuri wetu uko wapi? Kwa nini tunaiogopa Iran. Ukiona mchele umewekwa Kur`ani, hiyo Kur`ani si unaitupa tu, halafu unakula mchele?,`` alisema Membe. ``Tuiache Israeli iiogope Iran. Tuna ubalozi wa Iran, hatukuwafukuza. Kwa nini tunaogopa na jeuri zetu. Uamuzi huu utafanywa na Watanzania wote, serikali kazi yake ni kutoa changamoto. Naomba Watanzania tujiamini. Hata Tanzania tunachukiwa kwa kuishambulia Uganda, lakini tulikuwa na sababu. Kama (serikali) tungekuwa na woga tusingejiunga na Marekani kwa sababu hawa (Marekani na Iran) ni maadui,`` alisema Membe.
Waziri Membe alipotakiwa na waandishi wa habari katika viwanja vya Mnazi Mmoja muda mfupi baada ya kuhudhuria sherehe za �Siku ya Umoja wa Mataifa (UN)``, kueleza msimamo wake kuhusu kauli ya maaskofu ya kumtaka ajiuzulu, alisema: ``Sina taarifa, hivyo unavyoniambia ndio ninasikia.`` Alipoelezwa kuwa ndivyo maaskofu walivyosema wakimtaka ajiuzulu, Waziri Membe alisema: �Siwezi kwa sababu siamini.``

Source: Nipashe


WAPENDWA WANA SAYUNI.SISI KAZI YETU NI KUOMBA TU.LEO TUPO SIKU YA TANO YA MAOMBI YETU.NENO LA KUSIMAMA NALO NI LILE LILE LA 2NYAKATI 7:14.KAMA UNAPENDA KUUNGANA NA SISI KUHUSU MAOMBI HAYA TUANDIKIE KWENYE EMAIL HII: MIWLC@YAHOO.COM

if my people, who are called by my name, will humble themselves and pray and seek my face and turn from their wicked ways, then will I hear from heaven and will forgive their sin and will heal their land. Now my eyes will be open and my ears attentive to the prayers offered in this place.

No comments: