Saturday, October 25, 2008

Serikali yatoa tamko kuhusu OIC:MAOMBI MLIMA SAYUNI:TUPO SIKU YA NNE

Serikali imefafanua kwamba haijaamua kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC). Ofisa Mwandamizi wa Serikali aliiambia HabariLeo jana kwamba uamuzi wowote kuhusu suala hilo utawahusisha Watanzania, lakini bado hakuna uamuzi ambao umechukuliwa. Hatua hiyo imekuja baada ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), kumtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ajiuzulu wadhifa wake wa kisiasa iwapo ataendelea kupigia debe suala la Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC). Membe akizungumza juzi na wanahabari alionyesha kushangazwa na hatua ya baadhi ya Watanzania kuogopa Tanzania kujiunga na OIC. Waziri huyo alifafanua kuwa Tanzania haijajiunga na OIC, bali iko kwenye mchakato wa kufanya hivyo. Alifafanua kuwa hata hivyo suala la Tanzania kujiunga ama kutojiunga na OIC liko mikononi mwa Tanzania. Alisema makundi yote ya wananchi watatoa mawazo yao hivyo kwa sasa hakuna haja ya kuogopa wala kuzusha mijadala isiyokuwa na manufaa kwa nchi. “Waziri anayesukuma suala hili, anatakiwa ajiuzulu aache kuzungumzia suala hilo, kwani wananchi wamewatuma kuzungumzia masuala ya OIC?” Alihoji Askofu Dk. Owdenburg Mdegela baada ya kusomwa kwa tamko la maaskofu wa CCT jana Dar es Salaam. Naye Askofu Dk. Steven Munga alisema wao hawasimamii udini, bali wanasimamia Utanzania na akafafanua kuwa baraza hilo linasubiri suala hilo lipelekwe bungeni ndipo na wao watajua cha kufanya. Dk. Munga alisema kitendo cha Membe kutoa mfano wa Uganda kuwa inanufaika na OIC hakina manufaa kwani Watanzania ambao alisisitiza hawana cha kujifunza kwa taifa hilo ambalo alidai limegubikwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu. Askofu Sylvester Gamanywa alidai pingamizi la CCT sio la chuki kwa Uislamu ila ni pingamizi la kuzuia mgawanyiko wa kitaifa iwapo taasisi kama OIC itaingizwa kwenye mamlaka ya nchi. Pingamizi hilo lililosainiwa na Mwenyekiti wa CCT Askofu Mkuu Donald Mtetemelwa, walidai endapo nchi itaingia katika OIC, Katiba itakuwa imevunjwa na Watanzania wataingizwa katika migogoro itakayoua maridhiano, mshikamano, amani, utangamano na umoja wa kitaifa.
Source: Habari Leo

WAPENDWA WANA SAYUNI.SISI KAZI YETU NI KUOMBA TU.LEO TUPO SIKU YA NNE YA MAOMBI YETU.NENO LA KUSIMAMA NALO NI LILE LILE LA 2NYAKATI 7:14.KAMA UNAPENDA KUUNGANA NA SISI KUHUSU MAOMBI HAYA TUANDIKIE KWENYE EMAIL HII: MIWLC@YAHOO.COM

if my people, who are called by my name, will humble themselves and pray and seek my face and turn from their wicked ways, then will I hear from heaven and will forgive their sin and will heal their land. Now my eyes will be open and my ears attentive to the prayers offered in this place.

No comments: