Monday, October 27, 2008

Mchungaji kortini kwa kuharibu mali ya kanisa

Mchungaji wa kanisa la Pentekosti, Mackdonard Mwakisambwe (46), mkazi wa Sinza, jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni, kujibu shtaka la kuharibu mali ya kanisa hilo. Inspekta, Bennet Kipasika, alidai mbele ya Hakimu Frednand Kiwonde kuwa mshtakiwa aliharibu kanisa kwa kuezua paa, kuchafua madhabau na kuweka mchanga sehemu ya ibada. Alidai kuwa gharama zote za uharibifu huo ni sh. 600,000, mali ya kanisa hilo. Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo, Oktoba 15 mwaka huu, saa 11:00 jioni huko Sinza. Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka na yupo nje kwa dhamana hadi Novemba 5 mwaka huu, itakapotajwa.

No comments: