Tuesday, October 21, 2008

KUPANDA MLIMA SAYUNI KWA AJILI YA TANZANIA

BWANA ASIFIWE SANA WAPENDWA.

TULITANGAZA MAOMBI HAPA MLIMA SAYUNI KUHUSU KUIOMBEA NCHI YETU HASA KATIKA MAMBO MAKUU HAYA MATATU.
1.SUALA LA OIC
2.SUALA LA MAHAKAMA YA KADHI
3.SUALA LA AMANI YA NCHI YETU.

MAOMBI NDIO NJIA PEKEE AMBAYO SISI KAMA WATU WA MUNGU TUNAWEZA KUITUMIA KATIKA KUTAKA MUNGU AFANYE YALE TUNAYOYATAKA KUHUSU NCHI YETU NZURI YA TANZANIA.

MAOMBI HAYA YALICHELEWA KUANZA HASA KWA KUWA TULIKUWA TUNASUBIRIA KUJUA TAREHE YA KUANZA BUNGE LETU ILI TUMWOMBE MUNGU AWAPE HEKIMA WABUNGE WETU WAWEZE KUAMUA MAMBO HAYA KWA MUHSTAKABALI MZURI WA TAIFA LETU.
KESHO TAREHE 22NA SISI WANAMLIMA SAYUNI TUNAAMUA KAMA ALIVYOFANYA ESTHER ALIPOINGIA KWA MFALME AHASUERO KUMWOMBA MUNGU KWA AJILI YA MAMBO HAYA.
MAOMBI YETU YATAKUWA NI YA KUFUNGA KWA WALE WATAKAO WEZA KWA MUDA WA SIKU 21 NA KAMA BWANA AKIKUWEZESHA WAWEZA KUFUNGA KWA KADRI ZA NGUVU ZA MWILI WAKO ILA HAKIKISHA KILA SIKU KABLA HUJAFANYA SHUGHULI YEYOTE ILE UNAMWOMBA MUNGU KUHUSU MAMBO HAYA KADRI BWANA ATAKAVYOKUWEZESHA.
KATIKA KITABU CHA ESTHER ,TUNASOMA KUWA MODEKAI ALIMWAMBIA ESTHER KUWA KAMA WEWE USIPOFANYA ZAMU YAKO USIDHANI KAMA MUNGU HATALETA MSAADA KWA ISRAEL KUTOKEA SEHEMU NYINGINE...NATAKA NIWAAMBIE WATU WA MUNGU WA TANZANIA...AMBAO MNASIMAMA KAMA ESTHER MAANA NAJUA WAPO MA ESTHER WENGI WANASOMA HABARI HII NA PENGINE WANASITA SISTA KUMLILIA MUNGU KUHUSU HABARI HII..BWANA ANASEMA KUWA .....ANAWEZA KULETA MSAADA KWA WATANZANIA KWA NJIA NYIGNINE KAMA MSIPOFANYA NA KUSIMAMA KWA ZAMU ZENU...HII HABARI NIMEIPENDA SANA KWANI ILITOKEA HUKU BARA HINDI (INDIA) AMBAKO NIPO KWA SASA.MFALME AHASUERO ALITAWALA SEHEMU KUBWA YA DUNIA KUTOKEA HAPA INDIA NA WANA WA ISRAEL WALITANGAZIWA KUANGAMIZWA KWA KUWA KUNA BAADHI YA WATU WALIMDANGANYA MFALME AHASUERO KUHUSU WANA WA ISRAEL HATA AKATIA SAHIHI WARAKA WA KUWAANGAMIZA WA ISRAEL.
LAKINI IKUMBUKWE KUWA MFALME AHASUERO HAKUWA MTU MBAYA ILA ALIPATA USHAURI MBAYA KUTOKA KWA JAMAA MMOJA ANAITWA HAMANI...UTASOMA ZAIDI KITABU CHOTE CHA ESTHER NA NDICHO KITAKUWA MSINGI MKUU WA MAOMBI YETU.
BIBLIA INASEMA KATIKA 2NYAKATI 7:14..IKIWA WATU WANGU ..WALIOITWA KWA JINA LANGU..WATAJINYENYEKEZA NA KUNITAFUTA NA KUNIOMBA ..NITAIPONYA NCHI YAO.....OOH HALELUYA......!
HUU NI WAKATI WA KUOMBA NA SI KULALAMIKA KAMA WAFANYAVYO WANASIASA..SISEMI KUWA SIASA NI MBAYA HAPANA...ILA NASEMA SISI KAMA WATU TUNAOMJUA MUNGU MAOMBI NDIO NJIA PEKEE YA KUBADIRISHA JAMBO LOLOTE...KAMA UNAPENDA KUUNGANA NA WANASAYUNI WENGINE KATIKA KUOMBA KWA AJILI YA HILI...HEBU TUMA EMAIL KWENDA MIWLC@YAHOO.COM na ANDIKA SUBJECT YA EMAIL YAKO "HIVI "KUPANDA MLIMA SAYUNI KWA AJILI YA TANZANIA"KWENYE EMAIL YAKO ANDIKA JINA LAKO KAMILI, UMRI, MAHALI UNAPOISHI KWA SASA,UTAIFA WAKO, JINSIA YAKO,NAMBA YAKO YA SIMU UKIPENDA, PIA ANDIKA KWA KIFUPI KUHUSU KUUNGA KWAKO MKONO MAOMBI HAYA YA MNYORORO...TUTAANZA MAOMBI HAYA KUANZIA TAREHE 22/10/2008 .
N.B: EMAIL ZITAKAZOTUMWA HAPA HATUTAZITANGAZA HAPA UBARIKIWE NA BWANA YESU KRISTO WA NAZARETH.
AMEN

if my people, who are called by my name, will humble themselves and pray and seek my face and turn from their wicked ways, then will I hear from heaven and will forgive their sin and will heal their land. Now my eyes will be open and my ears attentive to the prayers offered in this place.

1 comment:

Anonymous said...

Shalom wandugu wote!
Kwweli kabisa, jukumu hili ni letu na bila kuomba hapa Tanzania hatutampendeza Mungu, tupo pamoja katika maombi haya na kuinenea mema nchi yetu wote.
Nawahimiza waombaji wote tuungane.
Kazi yako ni ya baraka Mtade.
LEMA