Tuesday, July 1, 2008

PHAUSTIN AENDELEA KUMPEPERUSHA YESU KWENYE RIADHA UJERUMANI

SHALOM!


Hata sasa BWana amenishindia!!!!
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtumishi wa Mungu na mwanariadha wa kimataifa Phaustin Baha ambaye habari zake tuliwaleteeni hapa katika mlima wa Sayuni tarehe 4 June, 2008, Bwana amemuwezesha kwa mara nyingine tena kuipeperusha vema bendera ya YESU.


Mnamo tar 29.06.2008 Bwana alimtendea muujiza mwingine kwa kumuwezesha kushika nafasi ya pili katika mashindano yaliyojumuisha wakimbiaji mbalimbali wa kimataifa 4650.
Mbio hizo zilifanyika katika jiji la Hamburg, Ujerumani na miongoni mwa wanariadha walioshiriki walitoka nchi zenye rekodi ya kuwa na wakimbiaji vinara ulimwenguni. Nchi kama Kenya, Ethiopia, Morroco, ulaya na sehemu nyingine za ulimwengu ziliwakilishwa katika mashindano hayo.

Binafsi Phaustin Baha anasema:
"...Katika nchi ya Ujerumani ilikuwa furaha tu maeneo ya HAMBURG :Kwa Mimi Phaustin Baha kuipeperusha bendera ya Bwana Yesu na NCHI YANGU TANZANIA KUWA MSHINDI WA (2) KATI YA WAKENYA ;ETHOPIA MOROCO NA NCHI NZINGINENASEMA ASANTE BWANA YESU KWAKUNITETEA: HALELUYA ?????? ..."

Nasi wana blog tunamrudishia sifa na utukufu Bwana Yesu na kuendelea kumtia moyo mtumishi Phaustin Baha ili aendelee kuipeperusha vema bendera ya YESU kote ulimwenguni.
Wapendwa wote nawasihi tuzidi kumombea Phaustin ili aendelee kukua vema kiroho na kumtetea Yesu katika maeneo yote anayopitia haswa katika ulimwengu wa riadha.
Ndugu yetu atakuwa safarini kurejea nyumbani Tanzania akitokea Ujerumani ndani ya wiki hii na hivyo basi maombi yako ni muhimu ili Bwana amfunike katika safari nzima ya kurejea nyumbani.

NB:Picha zote unazoziona hapo ni kulingana na ushindi wake wa tatu alioupata tar 24.06.2008.

1 comment:

Anonymous said...

Yap Kijana, huyo ndiye Yesu uliyempokea. Ukimuamini yeye hufanya njia kwako, kila kitu ni rahisi kama unamjua unayemuamini. Mungu wetu tunayemuamini hata sasa anatushindia, tunakua washindi kwa kua yeye anatuwezesha. Watu hawaelewi jinsi ya kuziamini nguvu za Mungu. Tukitambua hatutakua mikia bali tutakua vichwa!