Tuesday, July 22, 2008

VITA YA KIDINI UKRISTO NA UYAHUDI, ISRAELI.

Hii ni habari ambayo inaweza kumshangaza kila mmoja asikiaye na kuisoma. Lakini ndo ukweli halisi kwamba hata sasa Ukristo (Christianity) na dini ya kiyahudi ni vitu viwili visivyofungamana.

Wayahudi kupitia vipeperushi vinavyoweka kwenye magari, nguzo za simu na maeneo mbalimbali ya matangazo wamekuwa wakiupiga vita ukristo ndani ya nchi yao. Kwao ukristo ni sawa na imani potofu. Vipeperushi hivyo vimekuwa vikisomeka katika hali ya kuwatahadharisha watu kutokana na wale wenye jitihada za kuuneza ukristo: "Beware! These are the members of the Jewish Missionary Cult. They are baptizing Jews into Christianity." Ndani ya Israel nchi ambayo wengi tungetaraji iwe na wakristo wengi, lakini wakristo ni kati ya 6,000 na 15,000 tu.

Wengi tungelitaraji kwamba Israeli iunge mkono Ukristo lakini sivyo. Na hii yote ni kutimizwa kwa maandiko kwamba hata sasa kwao Masihi bado hajafunuliwa na wanamtarajia Masihi mwingine wakati ukweli ni kwamba Yesu Kristo alikwisha kuja nao wakamkataa ikiwa ni pamoja na kumsulibisha.
Waenda kwa miguu wakipita kando ya ukuta wa mji mkongwe wa Jeriusalemu.

Habari za hivi karibuni zinaonesha kwamba mchungaji mmoja David Ortiz, kutoka maeneo ya Ariel, Israeli na ambaye yuko mstari wa mbele kueneza injili alitegeshewa bomu la kutengenezwa kwa mkono kwa mfano wa kifurushi cha zawadi na ambalo lilimjeruhi vibaya mtoto wake baada ya kulitegua wakati akitoa chocolate.

Wengi wa wapinzani wakiwamo waalimu wa dini ya kiyahudi na kanisa la ORTHODOX wanasimamia vigezo kwamba kuruhusu kusambaa kwa Ukristo ni kutimiza unabii na kumfanya Kristo aje mapema.

Mstahiki meya wa mji wa Or Yehuda, mji ulio karibu na Tel Aviv aliamuru kukusanya na kuchoma biblia zote za agano jipya baada ya kuwaona wakristo (”Messianic Jews” kama wajulikanavyo huko) wakigawa biblia kwa wayahaudi wenye asili ya Ethiopia (KUSHI). Mambo hayo ya kunyanyaswa kwa wakristo yanafanyika pia katika miji mingine mingi tu ndani ya Isreali.

Israel na uongozi mzima wa nchi hiyo umejikuta katika hali ya kukanganya kwani kwa upande mmoja imekuwa mstari wa mbele kukaribisha mahujaji wa kikristo kutoka maeneo mbalimbali ya dunia na kwa wakati huohuo ikishuhudia ugandamizaji mkubwa wa haki za binadamu – wakristo kunyanyaswa ndani ya nchi hiyo. Naam pia imekuwa mstari wa mbele katika kujaribu kupinga wamisionari kueneza injili ya Kristo ndani ya israeli.

Inasikitisha kuona taifa hili ambalo ni chanzo cha wakristo wengi duniani kuwa katika hali ya namna hiyo. Na tuendelee kuwaombea wale wachache walioamua kuyatoa maisha yao kwa Kristo ndani ya nchi hiyo ili Kristo ajapo waende nae. Kweli wanatakiwa kusimama maana mazingira yao ni magumu kwani hakuna adui aliye mbaya kama wa nyumbani mwako.

1 comment:

Anonymous said...

Probably I can say with this blog make, more some interesting topics.