Wednesday, April 16, 2008

Askofu Kakobe na miujiza ya kuangusha watu

SOMO KAMA LILIVYOFUNDISHWA NA KAKOBE
"Somo letu la leo ni jipya kabisa katika mfululizo wa vipindi vyetu ambavyo tumekuwa tukiwaletea ndugu watizamaji kwa njia ya TV. hapo kabla kwa kipindi kama cha miaka 5 tulikuwa tukifundisha watu kama watoto wachanga...Na tulikuwa tukikazia zaidi uokovu. watu waache Dhambi na kuokoka.tunaweza kuona kwamba mtoto mchanga anapozaliwa kwanza anapata maziwa...chakula laini laini halafu anavyo kuwa anaanza kupewa chakula kigumu.Mpendwa mtizamaji bila kupoteza muda hebu ungana nami katika kipindi chetu cha leo ambacho somo ni juu ya MIUJIZA YA KUANGUSHA WATU CHINI.
Miujiza nini nini?
Katika biblia tumekuwatukiona mambo mbalimbali ambayo huonyesha nguvu za Mungu na kadhalika.Mambo mengi yalifanyika kimiujiza, au tunaweza kusema Nguvu za Mungu.Lakini hivi leo kumeibuka neno jipya linaitwa UPAKO.Jambo hili siku hizi limekuwa maarufu sana ambapo tumeona likitumika kwa watu wanao fanya miujiza.mtu anasema anagawa upako...watu wanakwenda kwa mtumishi (Labda mwinigine atajiita hivi mwingine vile.)utaweza kuona watu wananyoosha mikono na kutamka maneno fulani fulani. mara POWER au utasikia TOUCH. Na... utaweza kuona watu wakianguka chini.jambo hili limekuwa likikuwa siku kwa siku hapa Tanzania na limekuwa likivitua watu wengi.utaweza kuona mtumishi anakmkumbatia mwanamke na kugusa matiti yake anasema anamuambukiza upako! jambo hili linatoka wapi.Kuna kitu hapa... Kuna kituuuuuuu!!!!!
Au mtu anamkanyaga mtu tumboni na kiatu anasema anamuombea,uchafu wa namna gani huu!!??Kuna msemo wa kiingereze unasema POWER MUST COME AFTER PURITY.
Au utakuta mtu anamtaja Mungu kama vile mjomba wake!!!
JINSI YA KUPAMBANUA ROHO
1.JOHN 4.
Lazma tujua kwamba kuna roho ya Kweli na roho ya upotevu[1] Beloved, believe not every spirit, but try the spirits whether they are of God: because many false prophets are gone out into the world.
Sasa tunawezaje kuzijua roho hizi.Biblia inasema mtawatambua kwa matunda yao.utakuta watu hawa wanapofanya miujiza yao ya kuangusha watu. Huangusha kila mtu. wenye mapepo, wachungaji, wanakwaya, wote ambao ni wasafi. na utakuta mtu akiisha angushwa labda ndo waanasena wamemtoa pepo halafu baada ya maelezo fulani pale anaangushawa tena na tena.Roho gani ya Mungu iwaangushe wachungaji wa Mungu.au utakuta watu hawa hupenda kujiinua na kudai Mimi Mungu ameniambia anataka kunitumia kuliko mchungaji yeyote hapa Tanzania.na tena tunaweza kuona jinsi watu wanavyo fanya mambo haya kama maonyeshowanafanya nguvu za Mungu UPAKO kuwa ni maonyesho kama sinemaili watu waje kuona na kuvutika huko.je maandiko yanasemaje kuhusu nguvu za MunguNguvu za Mungu hazuji kwa ajiri ya maonyeshotukiangalia Musa tunaona alipasua maji si kwa ajiri ya maonyesho ila tu kwa ajiri ya tatizo ambalo liliwafikana pia wale kware waliokuja kule jangwani ni kwa ajiri watu hawakuwa na jinsi kuhusu chakula.pia Mungu alitumia nguvu zake mbele ya Farao ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye aliye ntuma Musa kwake.watu wamekuwa wakivutwa na hizi nguvu huku na huku.tusiishi kwa kuangalia Marekani.mwaka 1990 alikuja mtu kutoka marekani anajiita Nabii kufanya semina. tukaenda pale na mimi nilikuwa mmjo wa wale tuliokuwa pale jukwaani. sasa akaaanza hizo POWER...TOUCH huku akimyoosha mkono wake watu wanaanguka chini hata huku jukwaani kulikuwa na maaskofu na viongozi mbalimbali nao chini.akaanza kuwa kama ananisogelea nikasema (moyoni) haanguki mtu hapa, ntaanguka vipi sina pepo.mimi peke yangu ndo sikuanguka pale jukwaani
HIZI NGUVU ZINATOKA WAPI.Nakumbuka mwaka mmoja nilikuwa katika kufunga na kuomba.nikapata maono yakiniambia hivi. nenda kajiangalie kwenye kioo. nikaenda. halafu sauti ikaniambia weka mkono wako usoni nika weka kujitizama uso ukabadilika.halafu nikaonyeshwa watu kwenye kioo nikaona watu. nikaambiwa nyoosha mkono wako nikashosha watu wale wakaanguka, nikipeleka huku wanaanguka. nikaambiwa nitakuwa nambadili nyuso za watu.sasa nikaambiwa fanya mkutano ita viongozi mbalimbali halafu nataka ukaonyeshe nguvu zangukweli niakwaambia watu wakaandaa sehemu na ukumbi na watu wakaitwa wengine wakubwa kabisa na hata upinzani haukuwa mkubwa. mwaliko uliukuwa mkubwa.siku niliyotaka kwenda sasa, ghafla sauti nyororo ndogo ika niita na kuniambia KAA CHINI, Utapotea huko unakopelekwa si kwa ajiri ya kunitumikia mimi.niaahirisha na kuacha kabisa.leo hii watu wanavutwa na nguvu za upako na kupelekwapelekwa kusikojulikana na wengine wanatamani nao waangushwe.mwenye maonyeshpo ni shetani. alimpandisha Yesu Juu na kumuonyesha milk za Dunia.
MUNGU NI WA KUAMINIWA SI WA MAONYESHO NA MIUJIZA HAITAMPELEKA MTU MBINGUNI.WATASEMA SISI TULITOA PEPO KWA JINA LAKO NAYE ATASEMA ONDOKENI KWANGU SIWAJUI"MWISHO WA KUMNUKUU

Source:JamboForums.com @ JamboForums.com

7 comments:

Anonymous said...

kuna mtu amelengwa hapa..maana wenye mizaha ya madhabahuni ni wengi na kukumbatia wanawake wa watu wapo.

Anonymous said...

UJumbe umefika japo kuna maswali mengi sana kwa mhubiri, maana inaonekana neno POWER NA TOUCH NI MATATIZO, MAANA THEORY HII ANAYO PIA KULOLA, may be ni harakati za Kakobe kusafisha jina kwa kulola, maana kama kuanguka kuna watu huwa wanaanguka pasi hata kutamkwa neno power na Touch.

Mlengwa hapa si mwingine ni Maboya amabye kwa muda mrefu amekuwa hana uhusiano mzuri na Kulola, ikumbukwe hawa wote ni watoto wa Kulola.

NIMEULIZA MARA NYINGI NA NAOMBA MTU NISAIDIE HAPA, TATIZO NI MANENO POWER NA TOUCH, AY NGUVU ILIYO NYUMA YAHAO WATU.

MAANA POWER=NGUVU
TOUCH-KUGUSA.

MTU WA KAWAIDA PASIPO KUINGIA ROHONI HAWEZI KUELEWA. NAOMBA KAOKEB, KULOLA AU MTU YEYOTE AFAFANUE NA AELEZE IN DETAILS HAO WATU WANAPATAJE HUO UWEZO??? KUNA SIRI GANI HAPA.

AU WIVU??

WACHUNGAJI WANAOKUMBATIA WANAWAKE KWELI WAKO WENGI, WAMEJAA VITUKO VITUPU, HII NI AIBU TUPU.

KUNA HAJA YA KANISA KUJUA MBINU ZOTE ZA ADUI, SIYO BY SIMPLE WORD POWER NA TOUCH.

Anonymous said...

Katika watumishi ambao huwa wananihudumia Roho yangu vizuri,basi Kakobe ni mmoja wapo.Lakini hapa bado sijamuelewa vizuri Kakobe,tatizo ni nini,watu kuanguka au?,maana hata yeye huwa anaombea watu wanaanguka.Hata katika matangazo yake kabla kipindi hakijaanza tunaona akimgusa mtu halafu anaanguka.Sasa tatizo ni nini?.Roho amegawa vipawa mbalimbali kwa Watumishi wake,mbona yeye huwa anafanya miujiza mingine ya ajabu,kwa mfano kuombea wenye Vigugumizi,wenye Mba n.k.Mmmh kwa kweli hizi Siku za mwisho inabidi kuwa makini sana.....Ni bora kuomba Mungu atufunulie kujua watumishi wa Mungu wa Kweli.Tusije jiingiza katika mitego ya Shetani.

N.B,Sasa hivi kuna mlipuko wa jiji la Dar kuwa na WATUMISHI WA MUNGU WENGI,na hivyo waumini kutangatanga kutoka Kanisa moja kwenda lingine,inawezekana mafundisho kama haya yanalenga kuwalinda Waumini wasikimbie.Maana nilishakuwa muumini wa Kanisa fulani,ambapo Mchungaji Mara kwa mara badala kufundisha waumini wake neno la Mungu,basi yeye ataanza kuwasema watumishi wengine kuwa wana Roho za kipepo.Sasa sidhani kama mambo kama haya Yanakubalika ki-Mungu,ni bora Kuomba Mungu amuondoe mtumishi fulani katika upofu alionao kuliko kusengenya..

...........NI MAONI TU......

Anonymous said...

hapa aliyelngwa ni mtume wa efatha, mwingira.maana na yeye kwa kufanya mizaha mimbarani na kukumbatia wake za watu na mabinti ndo mwenyewe

Anonymous said...

Tehehehehehe! Kweli injili imevamiwa na maharamia! Yaani mtumishi anapata kumbatio la mke wa mtu? Thubutu amshike wa kwangu!! Itakuwa kasheshe hapo!!!

Anonymous said...

Mungu atusaidie na utitiri huu wa watumishi wa Mungu,mimi sijui hata niende kwa nani? Kwani ili kuwatambua kwa matunda yao inahitaji uwe na roho wa Mungu na si utashi.Mweeh !

Mary Damian said...

Hapo hapo! kuna kitu sio bure! WAPENDWA TUSAIDIENI KUELEWESHWA HAYA MAMBO