Tuesday, April 8, 2008

Ni "WALOKOLE" au "WAPENDWA"?

Kwa kila ampendaye Yesu, BWANA ASIFIWE!!

Nina mada ndogo tu ambayo nahitaji sana michango yenu haswa ewe msomaji wa makala hii.
Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi, hivi ni nini asili ya mtu/watu walioamua kumpa YESU maisha yao (KUOKOKA) kuitwa MLOKOLE/WALOKOLE?? Neno hili asili yake haswa ni kabila gani au wapi? Kwa kiingereza watu hao walio-okoka wanaitwa (born Again) na mfuasi wa imani ya kipentekoste ni mpentekoste, sasa MLOKOLE ni nani? Au ulokole nini? Je mpentekoste ni mlokole au ni zaidi ya hapo?

Sambamba na hoja hiyo hapo juu naona kuna neno jingine ambalo linajipenyeza taratibu, si baya katika kanisa, nalo ni "WALOKOLE" hao kujiita/kuitwa "WAPENDWA" /"MPENDWA" Neno hili hata blog yetu imelitohoa na kulitumia kama lilivyo. Hili neno nalo limekaaje ndugu zangu? Je hili neno "MPENDWA" nikilitumia kwa ndugu yangu asiye "mlokole" ni sawa?

Nauliza hivyo kama kichokoo tu ili tuwekane sawa haswa katika matumizi ya haya maneno!

Wafuasi wa kwanza wa injili ya YESU KRISTO iliyokuwa ikinenwa na mitume kuitwa "Wakristo" ilikuwa huko Antiokia. Sasa na walokole je?

Acts 11:26, "...and when he found him, he brought him to Antioch. So for a whole year Barnabas and Saul met with the church and taught great numbers of people. The disciples were called Christians first at Antioch..."

2 comments:

Anonymous said...

Mtumishi Maranatha,
Ni kweli kuwa neno walokole ni limekuwa ni maarufu sana hasa miongonimwa jamii yetu ya east afrika.Kwa kifupi ni kuwa asili ya neno hili ni uganda ( baganda) na wao walikuwa wanalitumia mwanzoni mwa miaka ya 1940,50 hadi 60 wakiwaita waumini wenye msimamo mkali wa kikatoliki (karismatiki) kwa wakati huo.Hao wakarismatiki walikuwa wanajiita abalokole liliwa na maana watu waliokoka au ongoka kama lilivyokuwa linatumiwa na wakatoliki wa watanzania miaka hiyo hiyo.Na walikuwa na salam zao wakikutana wanasalimiana kwa kugonganisha vifua na kuruka juu baada ya kugonganisha hivyo vifua.Wanawake walikuwa wanavaa magauni marefu sana hadi chini na walikuwa wanafunika vichwa vyao kwa vilemba vyeupe.
Kitu kimoja noticable kwa jamii hii ni kuwa walikuwa hawapendi kufanya kazi ila wala kujishughulika na kutafuta mali wakiamini kuwa hayo ni mambo ya ulimwengu.hali hiyo ilipelekea wengi kuwa maskini sana kiasi cha kuwa wahitaji wakubwa.Muda mwingi waliutumia kushuhudiana wao kwa shuhuda mbali mbali na walipenda kutumia neno kutendeleza wakati wakikutana kwenye kitu kinaitwa faragha.
So jamii hii ilikuwa kwa kasi sana hata watu wengine wa afrika ya mashariki hasa Tanzania waliojitangaza kuokoka waliitwa "walokole" na jamii ya wasioamini.Lakini ikumbukwe kuwa jamii hiyo ya wasioamini iliwaita hivyo kama kwa namna flani ya kuwadharau na kuwakebehi.Hivyo basi kila aliyeokoka miaka hiyo ya 50,60,70 hadi 80 aliitwa "mlokole" kwa kebehi ya wale wasioamini.Waliwaita hivyo wakiwafananisha na jamii hiyo ya wakarismatiki wa uganda ambao walipata sana nguvu baada ya mauaji ya "mashahidi wa uganda".
Neno hilo hapo mwanzo hapa Tanzania waamini wengi hawakulipenda kabisa ila kadri miaka ilivyokwenda ndivyo jamii ya waliokoka walipoanza kulikubali na kulioana la kawaida hasa pale watu walipokuwa wakikebehi kuwa "walokole" huwa wanalia kanisani. Hali hiyo ikawa kama ni kumwagia petrol kwenye moto kwani waliokoka wakalipokea kwa nguvu sana na kuanza kulitumia kama utambulisho wao kwa jamii nyingine ya wakristo.Utakuta mtu anasema "kwa hiyo wewe ni mlokole...ndio mimi ni mlokole bwana...!".
Kwa kifupi neno la kwanza kabisa kuwatambulisha watu wanaomfuata Yesu mara ya kwanza kabisa lilikuwa ni "wafuasi--likijumuisha kila mmoja aliemwamini YESU" au "wanafunzi likimaanisha wale waliomwamini YESU lakini likitumiaka kuonyesha aidha wale 120,au wale 500 au wale 70 au wale 12" na neno jingine lilikuwa ni thenashara hili lilitumika kwa wale 12 tu.Baada ya YESU kufa na kufufuka waliomwamini walitambulika kama watu wa njia ile na baada ya Matendo 13 huko Antiokia ndipo wanafunzi waliitwa kwa mara ya kwanza wakristo.
Lakini ikumbukwe kuwa neno wakristo halikuanza kutumika hapo Antiokia bali ukisoma Marko 9:41 "Mtu yeyote atakeyewapeni kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu ninyi ni watu wake Kristo [ ninyi ni wa Kristo], hakika hatakosa kupata tuzo lake" utaona kuwa neno wakristo linatumiaka hata kabla Yesu hajafa msalabani na kufufuka.
Kwa kumalizia niseme kwamba Neno walokole/Waliokoka/Wapentecoste (linalomaanisha watu wenye kuamini ujazo wa Roho Mtakatifu/kunena kwa lugha/Karama za uponyaji/Matendo ya miujiza/ubatizo wa maji mengi na maisha matakatifu),wakristo na mengine yanayofanana na hayo vyovyote yatakavyotumika inaweza isiwe jambo kubwa sana ila kikubwa ni mtu kuwa na uhakika wa kuingia mbinguni.
Naomba nimalizie hapo kwanza niache wachangiaji wengine waendelee.

By Utade