Wednesday, April 23, 2008

H.Clinton kambwaga Obama in Pennsylvania

Seneta Hillary Clinton amemsinda Seneta Barak Hussein Obama huko Pennsylvania.
Majuzi wakati wanahojiwa na waandishi wa habari kuhusu msimamo wao kama Iran itaishambulia Israel Seneta Clinton alisema kuwa akiwa rais atahakikisha kuwa America inajibu mashambulizi kwa kipigo kikali kuiadhibu Iran.Lakini senator Hussein Obama alisema kuwa akiwa rais kama Iran itaishambulia Israel yeye ataangalia njia muafaka wakati huo.
Obama ni mwafrika mwenzetu tunapenda awe rais ila Clinton ameonyesha mwelekeo mzuri juu ya Israel.Ndio maana nawapenda republican kama akina G.Bush maana wao sera zao juu ya Israel zipo wazi kabisa kuwa atakayeigusa tu atapata kipigo kikali.Naona na bibi Hillary Clinton naye ameanza kuonyesha positive direction kuhusu hilo.
Hata hivyo ningependa Hussein Obama awe rais wa Marekani ila kuhusu Israel napenda kuona ameweka wazi sera zake.


4 comments:

Anonymous said...

Mtade,
Inaonekana unaonesha jinsi ulivyo mwizraeli kwa imani. Mungu mwenyewe amesema atakayemgusa mwizraeli cha moto atakiona.Nadhani hatuhitaji wala kuwasaidia, ni kwamba Mungu mwenyewe ajua jinsi ya kuwatetea watu wake. Hivi unajua Mtade kuwa wapo maadui wengi wanaokuzingira, lakini Mungu huwakatilia mbalii! ndivyo ilivyo kwa taifa lake israeli,,Na tuwatakieni amani wayahudi wote halisi na Mungu atatubariki.
Sauti ya Nyika.

Mtade said...

Ni kweli Sauti ya nyika mimi ni muisrael kweli kweli na ndio maana nipo makini sana na habari za aina yoyote zinazoihusu Israel kwani kuja kwa YESU kulichukua kanisa kunategemea sana position ya Israel.
Ubarikiwe.
Mtade

Maranatha said...

Mtasema yote wapendwa lakini lazima maandiko yatimie. Lazima Isreli ishikishwe adabu ili wajue kwamba YESU (masihi) alikuja kwa ajili yao na wao wakamkataa ikiwa ni pamoja na kumsulibisha kwa mauti ya aibu.

Kama Obama ataisupport Israel au la Mungu ndiye ajuaye kwani anamuita Nebukadreza mfalme wa Irani(Uajemi zama za agano la kale) mtumishi wake, si kwa sababu ni Muisraeli bali alitumika kama chombo cha kuwatia adabu Israel na kutimiza unabii wa Yeremia. Na sitashangaa ikitokea hivyo tena leo. Waliyomfanyia Kristo ni makubwa lakini alivumilia yote. Na hata mwisho alikiri Yesu mwenyewe kwamba Baba uwasamehe kwani hawajui walitendalo. Walialikwa kwenye karamu wakakataa kwenda, ikabdi aamue kuwakusanya wapita njia, viwete na walalahoi (mataifa).

Kwa hiyo wapendwa kwa suala la uchaguzi Marekani tuwaombee tu kwamba apatikane aliye kusudi la Mungu na si vinginevyo.
Iwe Obama, Clinton au McCain-Bwana Mungu ajitwalie aliye muafaka kwa kipindi hiki. Utashi na mapenzi yetu vyaweza kutupotosha! Ila lazima neno lisimame palepale kwani kama ni unabii hakuna kilichosalia zaidi ya injili kuhubiriwa kila pande ya dunia!

Maranatha - Bwana wetu anakuja!!

Anonymous said...

Obama ameanza kuniboa,kwanza aliwahi kuwa muislamu alipokuwa mdogo