Tuesday, April 1, 2008

TAREHE 1.APRIL - SIKU KUU YA WAJINGA DUNIANI!

Nashindwa kuelewa dunia inakoelekea na mlengo ambao imeamua kuuchukua kiasi kufanya vitu kinyume na hali halisi. Kidogo kidogo zile sherehe ambazo hapo awali hazikuwa na mvuto wala nguvu za kuvuta watu sasa ndo zinaonesha kushamri na kuwa na nguvu. Zipo sherehe ambazo ukifuatilia maudhui yake sipati jawabu la dhati ndani. Kwa mfano Happy Valentine na hii ya tar 1 april.
Nitaizungumzia kidogo sikukuu ya wajinga ambayo kwangu inaonesha dhahiri namna gani mwanadamu anavyojitahidi kuihalalisha dhambi kuwa kitu cha kushangiliwa. Siku hii watu wengi wameitumia kama kigezo cha kuhalalisha uongo kuonekana kuwa si dhambi. Naam hii imewakumbuka hata watu wa Mungu. Mtu anadanganya kisha anatoa kigezo ati leo ni siku ya wajinga, wapi yameandikwa hayo ndani ya neno la Mungu - Biblia?? Ni mchungaji gani kakufundisha uongo huo? Ni muhimu tukawa makini katika ushiriki wetu wa sherehe na sikukuu na haswa tutafute kujua chimbuko la sherehe hizo na mantiki ya kushiriki kwetu. TUSIKURUPUKE! Nachelea kusema kwamba nyingi ya sherehe hizo ni mkakati wa shetani kutaka kuwakosesha watu wa Mungu kiasi kwamba wengi wa waliofanya hivyo (wapendwa) sidhani kama huwa wanachukua hatua ya kutubu kwa dhambi hiyo ya uongo!!
Ni vizuri kuwa makini kwani dhambi zote ni sawa na hakuna dhambi kubwa wala ndogo mbele za Mungu. Na pia mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele, na pia sisi tulio watoto wa Mungu biblia yasema hatutendi dhambi na atendaye dhambi ni MUASI!!!
Hakuna siku kuu ya wajinga kwa waliokoka!!

2 comments:

Mary Damian said...

Tatizo la wapendwa ni MAZOEA na kusema kwamba tunakwenda na wakati! bila kujua kwamba sikukuu nyingine chanzo chake ni nini, mfano sikukuu ya wapendanao, na hii ya wajinga tufahamu kwamba baba wa waongo wote ni shetani, na sikukuu ya wajinga uongo unatawala sana na kama tujuavyo, sisi wakristo unapokiri kitu hutokea tayari tumejifungia baraka zetu, kwa sababu mshitaki wetu hayuko mbali. BARIKIWENI

Anonymous said...

Ni kweli kabisa ulichosema dada mary.Mungu akubariki kwa mchango wako.

Mtade (Baba Chinyemi)