Ramadhani Musa (18) anayedaiwa kuingia Dar es Salaam juzi akitokea Mtwara, amenaswa akiwa na kichwa cha mtoto mdogo. Mtuhumiwa alikamatwa na walinzi wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam jana asubuhi akijaribu kukipitisha kwa staili. Akiwa na kifurushi aliwahadaa walinzi kuwa anakwenda kumuona shangazi yake, hata hivyo walimshtukia baada ya kuona damu zimetapakaa mdomoni. Walipokagua kifurushi walikuta kichwa cha mtoto wa kike aliyekuwa amesukwa mtindo wa `twende kilioni` kikichuruizika damu. ``Kijana huyo alikichukua mbele ya walinzi hao na kuanza kufyonza damu na kujilamba midomo, `` alidai mlinzi na kuongeza kuwa aliwauliza kwa ujasiri mnashangaa nini? ``Kwetu ni kitu cha kawaida kula nyama za watu.`` Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala wa Bw. Charles Chambo, alithibitisha kutokea kwa mkasa huo na kueleza kuwa kichwa hicho ni cha Salome Yohana (3). Kwa mujibu wa mama Salome, Bi. Pendo Dutsan, binti yake alitoweka juzi usiku nyumbani kwa shangazi yake anayeishi Segerea na kwamba kabla ya kuishia alikuwa akicheza nje ya nyumba yao. Waligundua kuwa hayupo wakati wa chakula cha jioni na kuanza kumtafuta lakini bila ya mafanikio hadi jana asubuhi, mgeni wa jirani yao aliyetajwa kwa jina la Lucas Kibaya, alipogundua kiwiliwili chake chooni. Alidai Kibaya aliingia chooni na kukuta tofali limefunika tundu na alipoliondoa aliona kanga iliyokuwa na damu na kugundua kiwiliwili cha mtoto kilichonasa kwenye tundu hilo. Baada ya kutoa taarifa, polisi wa kituo cha Stakishari Ukonga walifika na kuopoa kiwiliwili hicho na kutafuta gari ili kunyonya uchafu ili kutafuta kichwa ambacho kilikuwa hakionekani. ``Wakati tunaendelea kukisaka kichwa polisi walitueleza kuwa walipokea taarifa za kukamatwa kwa Musa akiwa na kichwa Muhimbili,`` alisema mwanamke huyo akilia kwa uchungu. Aliongeza kuwa polisi walikichukua kiwiliwili pamoja kuwakamata watuhumiwa ambapo mwili huo ulikuwa chooni kwao hadi kituo cha Stakishari. Baada ya taarifa za kupatikana kichwa hicho, watuhumiwa ambao kiwiliwili kilikuwa nyumbani kwao walipelekwa Muhimbili hospitali walikoonyeshwa kichwa pamoja na `miliki.` Watuhumiwa hao Kibaya na mkewe Hadija Ali walimtambua kijana wao na kueleza kuwa alikuja Dar es Salaam Ijumaa, siku moja kabla ya tukio, akitokea Mtwara. Hadija alidai walitengana na mzazi mwenzake (baba wa mtoto huyo) kwa miaka mingi na muda wote alikuwa akiishi Mtwara. Alisema Ramadhan alitoweka juzi jioni na alipigwa na butwaa baada ya kuona kuwa aliyekamatwa na kichwa cha Salome ni mwanae. Mhudumu wa chumba cha maiti Muhimbili Bw. Mizome Gogo, alisema kichwa hicho kilifikishwa jana asubuhi na polisi na muda mfupi baadaye askari wa Stakishari waliwaletea kiwiliwili.
SOURCE: Nipashe
3 comments:
NIMEIFUATILIA HIYO HABARI,NA INASEMEKANA HUYO MTOTO ALISHAWAHI KUANGUKA KATIKA PAA LA KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD,MIKOCHENI.BAADA YA HAPO AKACHUKULIWA MPAKA KITUO CHA POLISI NA BAADAE KUPIMWA AKILI.ILA WAKAMWACHIA BAADA YA KUONA ANA AKILI TIMAMU(YALE YALE YA KUSEMA NI USANII UMEFANYIKA KANISANI).SASA MATOKEO YAKE NDIO HAYO,MTOTO KAGUNDULIKA MSHIRIKINA,LAITI WATU WA MUNGU WANGEMFUNGUA KATIKA VIFUNGO HIVYO,YASINGETOKEA HAYO.
NIMEIFUATILIA HIYO HABARI,NA INASEMEKANA HUYO MTOTO ALISHAWAHI KUANGUKA KATIKA PAA LA KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD,MIKOCHENI.BAADA YA HAPO AKACHUKULIWA MPAKA KITUO CHA POLISI NA BAADAE KUPIMWA AKILI.ILA WAKAMWACHIA BAADA YA KUONA ANA AKILI TIMAMU(YALE YALE YA KUSEMA NI USANII UMEFANYIKA KANISANI).SASA MATOKEO YAKE NDIO HAYO,MTOTO KAGUNDULIKA MSHIRIKINA,LAITI WATU WA MUNGU WANGEMFUNGUA KATIKA VIFUNGO HIVYO,YASINGETOKEA HAYO.
Maswali bado ni Mengi sana hapa??
1.Vyombo vya habari akiwemo kamanda wa polisi na hata Rwakatare walisema watoto hawa hawana wazazi, na hili wengi tulisema lifuatiliwe maana haiwezekani watoto hawa hususanu huyu akawa (melkizedeki) yaani hana baba wala mama?? Je hawa wazazi sasa wanatoka wapi?? maana wamekamatwa na wako ndani sasa hivi.
2.Narudi pale pale athari za kutangaza mambo haya bila Roho matakatifu.JE HUYU MTOTO ALIOMBEWA HILI HIYO ROHO IMTOKE, KAMA ALIOMBEWA JE AOMBEWE MARA NGAPI NDIO ROHO YA KICHAWI IMTOKE??
3.Je walokole wa kwa mama Rwakatare wanatambua kama mtoto huyu kweli alihitaji msaada wa Mungu wao ndio wana makosa.NI muumini gani wa kwa mama Rwakatare ambaye alimfuatilia huyu mtoto kipindi wanafanyiwa uchunguzi na madaktari, kipindi wamekamatwa na polisi, na walipoachiwa maana mtoto huyu ni wao! kwa nini walimuacham hakuna hata mmoja kati ya waumini 1000 kumfuatilia huyu mtoto??
4.JE ni hekima na ni kweli kwa akili ya kawaida mtoto kuwa mchawi pasi kugundu akuwa kuna watu wazima nyuma yake?? je zilichukuliwa hatua gani za kimwili na kiroho kufuatilia hilo HILI KUUKATA MZIZI WA UCHAWI?? maana hata kama huyu mtoto ataokoka, je atasimama katika wokovu.
5.Je mama Rwakatare anaweza akjivuna kuwa wakweli kusema kuwa huyu mtoto alianguka toka juu ya paa, huku kukiwa na maswali mengi ya kiroho na upungufu wa kutunza kondoo.
6.Je hakuna maono, manabii, hakuna aliyechukua mzigo wa mtoto huyu na familia yake ili afunguliwe??
7.Je tunajifunza nini katika hili??
Post a Comment