Tuesday, April 29, 2008

Maombi na maombezi kutoka sayuni

Bwana YESU KRISTO asifiwe sana....

Kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakinitumia maombi yao mengi kupitia mlima huu wa sayuni,ningependa kuwafahamisha kuwa muwe mnatutumia na namba zenu za simu katika email zenu ili kurahisisha mawasiliano.
Wengi wamekuwa wakipokea majibu yao mbalimbali kutokea mlima huu wa sayuni.Maana YESU KRSITO ni yeye yule jana,leo na hata milele."Waebrania 13:8".
Kumbuka kuwa unapotendewa muujiza wowote utukufu na sifa zote mpe MUNGU wa mbinguni,maana ni yeye anayestahili na sisi ni watumwa wake tu.Pia wakati unatuletea shuhuda zako naomba utueleze wazi kama ungependa tuweke ushuhuda wako hapa wazi ili wengine wajengeke.Kumbuka kuwa maombi haya ni siri kati mwanasayuni mwombaji na wewe mwenye shida,hivyo usisite kutueleza shida yako kwa kinagaubaga ili tuweze kukuombea kwa bidii mbele za Mungu wetu na utapokea majibu yako kama wengine wengi.

1Wakorintho 4:1-2 "Basi, mtu na atuhesabu sisi kuwa watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za Mungu."

Angalia maelezo na email zetu hapo pembeni kulia kwa maelezo zaidi.

No comments: