Tuesday, April 22, 2008

NINI TATIZO; VIMINI AU WATAZAMAJI WANAOPITILIZA MIPAKA YA KUWAZUA?


Siku moja nalikuwa kwenye ibada ndani ya kanisa mojawapo la Ki-Pentecoste hapo Dar Es Salaam, Tanzania. Siku hiyo akaja dada mmoja na nguo nzuri tu kwa namna yake. Kwa bahati mbaya sketi aliyovaa ilikuwa fupi na zaidi ya hayo kukawa na mpasuo kwa nyuma. Mpasua huo ulikuwa mushkeli kidogo kwa baadhi ya watu. Muda si muda wakati ibada ikiendelea Shemasi mmoja wa kike akamchoropoa yule dada toka ibadani na kumpatia kipande cha khanga ili walao kulinda staha. Sikuelewa kama nia ya yule dada ilikuwa ni kutumiwa na adui au kwake hilo halimkushtua.

Sasa leo katika soma soma yangu ya magazeti yetu nimekutana kisa kinachotaka kufanana na hicho. Ni pale baba paroko anapoamua kupiga marufuku uvaaji wa vivazi hivyo kanisani naam haswa wakati wa ibada kwa mintarafu kwamba vinawakwaza baadhi waumini.Hakuishia hapo ameenda hata kuruhusu kwa wadada hao kupewa huduma ya khanga pindi wanapogundulika kwamba vijivazi vyao, mhhh havina upako nyumbani mwa Mungu. Sasa sijui hizo khanga kama baada ya ibada wanazirudisha au ndo tuite muujiza kwao!

Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi, kwani tunapotembea mjini hawa watu tunakutana nao, tukiwa makazini tunao wewe ni shahidi, mashuleni ndo wanafunzi usiombe hivyo vijisketi utadhani ni sehemu ya chini ya jezi ya Netiboli. Lakini huko kelele sio nyingi sana kama inapokuja swala la hawa watu kuingia kwenye masinagogi. Sasa niulize jamii tatizo liko wapi? Kuvaa hivyo "VIMINI" au watizamaji wamekuwa wakitazama mpaka kujiumbia taswira ambazo hazipo? Na kama kweli tunakwazika tukiwa kanisani, je tukiwa mashuleni, ofisini, na mitaani huko tunakuwaje? Tunachekelea na kukubaliana na hali hiyo au? Na hili swala limekuwa likilalamikia zaidi na wanaume sijajua nini msimamo wa akina mama, hebu naomba mjisemee je nanyi mnakwaza? Na nini kinawakwaza haswa hapo? Najiuliza hivi huu si udhaifu wetu wanaume kwa kutokujua kufumba macho na kuyapa nafasi mambo ambayo si ya muhimu kuvamia ufahamu wetu? Uko kanisani inaendelea badala ya kutafakari neno unamkodolea macho dada au mama wa watu, je huu ni uungwana? Ayubu anasema "...Nilifanya agano na macho yangu, Basi nawezaje kumuangalia msichana? (Ayubu 31:1) Na Yesu anasemaje; "...Amuangaliaye mwanamke kwa tamaa amekwisha kuzini nae moyoni mwake..." (M athayo 5: 28).

Nina maswali mengi kuliko majibu hebu na tushirikishane na kusaidiana katika hili ndugu zangu!

1 comment:

Anonymous said...

Mtumishi wa Mungu hakika swali hili ni very challenging, na hatutakwepa kujibu kutokana na ufahamu wetu mbali mbali ktk hili swala nitajaribu kujibu kadiri Roho atakavyoniwezesha.

Nitafurahi na mwingine akijibu ili tuwe na majibu ya kutosha.

Biblia inasemaje??

‘’Vivyo hivyo wanawake na waJipambe
kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja
na adabu nzuri, na moyo wa kiasi;
si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu
na lulu, wala kwa nguo za thamani;
bali kwa matendo mema, kama
iwapasavyo wanawake wanaoukiri
uchaji wa Mungu ‘’ 1 timotheo2:9

Hii ni moja ya sababu ya kuipenda biblia!!! kila jibu lipo, akina dada wengi hawafuati hili andiko.

Nakumbuka kuna watu wameokoka kwa sababu ya mavazi ya walokole wanaume!!! walokole wanaume wanapendeza sana kwa mavazi yao kuliko wanawake(tujipongeze kwa hili).

Biblia hap juu inasema KWA WALE WOTE WANAOKIRI UCHAJI WA MUNGU, KINYUME NA HAPO SI UCHAJI WA MUNGU!!

Pengine ni kwanini inakuwa hivi.

1.Wasichana wanaovaa vimini na nguo fupi wametawaliwa na udunia, biblia inasema tugeuzwe nia zetu na mawazi yetu!!! Nia yao ni kupata wanaume, pengine wa kuwaoa au vinginevyo!! ukisha kuwa na mawazo kama haya huna Mungu, haijalishi unaimba kwaya au unatoa sadaka sana!! ukishakuwa unawafuata watu wa dunia hii wewe pia ni wa dunia na biblia inasema wazi wenyeji wetu ni wa mbinguni.

2.Wachungaji wengi ambao makanisa yao waumini wao wanavaa nguo fupi wamekosa ujasiri wa kukemea
kwani
(a)watapoteza kondoo! na kwa sababu wanawake wanaouhudhuria makanisani ni wengi kuliko wanaume, basi mchungaji hawana ujasiri tena, akikemea watahama na kwenda kanisa la jirani.
(b) pengine ni roho za kizinzi ambazo zimewaandama wachungaji wengi! , ndio maana wako radhi kukaa na muumini anayevaa kimini kwa sababu tu anakuwa anatamani kwa kuona(wako wanaomaliza)

3.Akina mama jukumu lao, kama tito inavyosema ni kufundisha mabinti(kwa lugha ya upole na hekima) wao wa kike namna ya kuvaa( hapa
nazungumzia kanisani)
Tuna akina mama ambao wao wenyewe wanashindana mavazi kila siku jumapili makanisani, pengine akina mamawengine wanatamani wangekuwa vijana lakini wanashindwa umri umeenda.

4,Katika familia level familia nyingi ambazo zinajiita za kisasa watoto wanenda bichi na kuvaa nguo za vituko kwa kusema eeti wameendelea! kumbuka huyu mtoto kesho ndio atakuwa mama naye!!!

5.Ni upofu wa kiroho, kwani kila sehemu na mavazi yake ktk dunia hii(sisemi kuwa kanisani watu wavae mavazi ya kusitiri halafu katikati ya wiki uvae mavazi ya ajabu la.

KUMBUKA MIILI YETU NI HEKALU WALA SI LILE JENGO!!!! PALE AMBAPO MWILI WAKO NA ROHO WA MUNGU VINAPOKUBALIANA LAZIMA TENDO LITAKUWA LA KITAKATIFU PALE AMABAPO, AKILI YAKO INAPOUWA KIONGOZI WAKO, BASI MUNGU ANAWEKWA KANDO.

WATU WENGI HAWATAMBUI KUWA MIILI YETU NI HEKALU LA ROHO MATAKATIFU.

6.JE ROHO ANAKUTUMA KUVAA MAVAZI MAFUPI?? TUMEAMBIWA KTK YOHANA KILA KINACHOONGOZWA NA ROHO HUYO NDIYO MWANA WA MUNGU.

KWA WANAUME!!!

Mtumishi kweli tunahukumiwa sana na kila sehemu hali iko hivyo, kweli kwa mtu aliyeokoka, sataili ya dunia ya leo ni kama Ayubu, kula yamini na macho yetu kutotazama kwa kuwaza--ukiangalia mara ya kwanza, kimbiza macho usiendelee kuangalia tena kwani ukiendelea kuangalia utavutwa na vitu vingine kwa hiyo.

1.Kuomba kwa nguvu tukitambua wavaao vimini siyo makanisani tu hata makazini na kila mahali!! hivyo Mungu tu atatuepusha.

2.Tukitambua kila avaae nguo fupi ni shetani'' hata kama ni bosi wako, jaribu kukemea akisikia shauri yake!!

3.Tujaribu kwa upole kuwaeleza kuwa nguo zao sio nzuri-kama mko ofisi moja n may be mko wawili tu(Mungu atusaide), maana kuna mazingira ukiyaachilia ayakaota mizizi mwisho wake ni kuanguka.JARIBU KUWA MKWELI, MAANA UZINZI TUNAUKIMBIA!!! si kila sehemu unakimbia, kama mko ofisi moja utakimbia kwenda wapi???


AKINA DADA MTUSAIDIE JAMANI '' JIFUNZENI KWA BATHSHEBA ALIMWANGUSHA DAUDI''

Mwisho :


Hakuna kisingizio kwa wanaume ndio dunia na inabidi tushinde.

Kalenge.