Sunday, April 13, 2008

Dereck - Gospel Music Producer

Wengi wanamfahamu kwa jina la Dereck,Ni mmoja kati ya maprodyuza wa siku nyingi sana hapa nchini wa muziki wa injili.Mbali na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza muziki na uchanganyaji mahili wa vyombo na sauti pia ni mpigaji wa vyombo vya muziki vya aina zote.Dereck ameanzia kazi ya muziki mkoani Mwanza miaka ya 80's na baadaye akahamia kanisa la EAGT mnazi mmoja.Wakati akifanya mahojiano na mlima Sayuni Dereck alimwambia mwandishi wetu kuwa kwa sasa anamtumikia Mungu kama mwalimu wa kwaya na mpiga muziki wa Faith Choir katika kanisa la Faith Word Church lililopo mnazi mmoja jijini Dar es salaam.Hivi sasa mtumishi Dereck amefungua studio yake binafsi inayoandaa na kutayarisha muziki wa injili inayopatikana maeneo ya mnazi mmoja.Anawakaribisha vikundi mbalimbali vya kwaya na waimbaji binafsi wa injili kumtembelea studioni kwake kwa huduma za bei nafuu na zenye ubora.
Unaweza kumpata +255-784-478340

5 comments:

Anonymous said...

ASANTE MTADE UMENIKUMBUSHA HUYU MTUMISHI WA MUNGU, MAANA TUMEABUDU NAYE SANA PALE MNAZI MMOJA ENZI ZA ANDREW, MASKINI KANISA LIKAVUNJWA KWA SABABU ZA KIBINADAMU SIYO MUNGU, NA DHAMBI ILE NAHISI ITAENDELEA KULITAFUNA KANISA HILI LA MNAZI MMOJA MPYA CHINI YA MWAKIBLWA, TULIKUWA JANGWANI TUKAAMBIWA WAUMINI WOTE WA MNAZI MMOJA WANATAKIWA WAAMIE MAKANISA MENGINE WASIENDE TENA KANISA LAO CHINI YA ANDREW, NAPENDA KUSEMA WAZI KILE KITENDO MPAKA LEO KIMENIUMIZA, MAANA SJAMPATA MCHUNGAJI KAMA ANDREW, NINAPOWAONA HAWA AKINA DERECK NAUMIA ZAIDI.

DERECK MUNGU AKUSAIDIE, NIMEFURAHI KUSIKIA UNA STUDIO YAKO.STUDIO NYINGI ZA DSM ZINAENDESHWA NA WAMATAIFA, NINA WADOGO ZANGU WENGI WAIMBAJI NIMEONA JINSI WAKINYANYASWA NA WASICHANA WAKIOMBWA MAPENZI.NA HILI SULA NINALIFUATILIA KWA KARIBU NA IKO SIKU WANASAYUNI NITAWAELEZA KIUNDANI.KUNA WAIMBAJI WA INJILI WANATAMBA SASA KAMA HAWAKUTOA RUSHWA BASI UZINZI.

KUNA STUDIO MOJA NIMESAHAU JINA(INAMTENGENEZEA NYIMBO BAHATI BUKUKU,CHIDUMULE NA (Ndshani ni FM studio) mmiliki wake hana tatizo ila kuna wafanyakazi wake (mmoja ana asii ya kikongo) anadai rushwa wazi wazi,mbali ya kulipia officially. usipo mpa nyimbo anatoa vibaya.kwa mwatu wanaoenda pale wanajua lazima apewe chake.

FM clouds hiyo ndiyo mmiliki wake ana tatizo, ni mmzinzi na vithibitisho vipo, amewaomba kufanya mapenzi na wasichana wengi tu.bila hivyo hautasikika.

mtade samahani nimeandika juu juu muda ukipatikana will give you full story.

NI KUWA TUWAOMBEE HAWA WALOKOLE WENYE STUDIO ZAO NI BORA KULIKO WAMATAIFA. TUOMBE TENA WASAMBAZAJI WAWE WALOKOLE HUKO KUSAMBAZA NDIO KUNA MATATIZO MNO.

Anonymous said...

Aaaghh mkulu Dereck! Naona mambo yako super siku hizi mzee! Kutoka gitaa, keyboard mpaka studio!! Endelea mbele na nakutakia kila la heri na mkono wa Bwana uwe pamoja nawe! Chalu (zamani Sinza EAGT, sasa niko shule Oslo Norway. Tuwasiliane mzee chalujohn@yahoo.com

Anonymous said...

huyu jamaa namkumbuka sana.niliwahi kusali naye bugando mwanza.kumbe alihama.

emmanuel mbalazi

DORAH said...

NILIKUWA muumini wa kanisa la EAGT MNAZI MMOJA..CHINI YA MCHUNGAJI andrew.naomba nifahamishwe kanisa hilo limehamia wapi..nikija TANZANIA NAHANGAIKA KUTAFUTA SEHEMU YA KUABUDU..NAOMBA TAARIFA.

Mtade said...

Mtumishi Dora, Kanisa la Pastor Andrew kwa sasa lipo mnazi mmoja kati ya jengo la ushirika lumumba na ilipokuwa sukita zamani.Kuna jengo jeupe la ghorofa saba.karibu kabisa na mabasi ya hekima au sumry yanayotokea mbeya.Ukifika hapo pandisha ghorofa ya tatu utakuwa umefika.Kanisa linaitwa faith word church.Kwa maelezo zaidi ukifika piga namba hii utafika 0713-427857

Barikiwa