Thursday, April 17, 2008

Injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu...
Maelezo ya picha:
Picha ya kwanza:
Mtumishi wa Mungu Farouk mwenye asili ya kiasia anayetabasamu baada ya kumpa YESU maisha yake akiwa na mjoli wa Bwana, Mtade
Picha ya pili:
Mtumishi Komba wa Kibaha wa kwanza kushoto akiwa na mjoli wa Bwana,Mtade.Hapo ni baada ya kumpa YESU maisha yake.
Picha ya tatu:
Mtumishi Komba baada ya kumpokea Bwana YESU jana usiku maeneo ya Kariakoo.
Picha ya nne:
Mtumishi Komba akiwa na mtumishi mwenzake farouk wakiwa wenye furaha baada ya kumpa YESU maisha yao.
Heleluyaaa...!
Jana jioni nikiwa katika pitapita yangu maeneo ya kariakoo katika utumishi huu nikaamua kujipumzisha makutano ya mtaa wa sikukuu na mkunguni ili nipate mishkaki na urojo.Kwa wale wenyeji wa kariakoo watakubaliana nami kuwa shehemu hizi za urojo wateja wakubwa ni ndugu zetu wahindi,waarabu,wapemba na watu wenye asili ya pwani.
Nilibahatika kuketi karibu na ndugu mmoja mwenye asili ya kiasia aliyekuja kujitambulisha kwangu kama ndg. Farouk anayeishi hapo kariakoo.Kama ilivyo ada yangu nikaamua kumshirikisha habari za YESU KRISTO wa Nazareth,haikunichukua muda na wala sikutumia nguvu nyingi maana nilimweleza upendo wa YESU ulivyo mkuu juu ya wanadamu.Ndipo ndg. Farouk akaamua kumpa YESU maisha yake (yaani akakubali kuokoka).Ikabidi nimwongoze sala ya toba mahali hapo hapo na baada ya maombi mafupi akawa mwenye furaha sana.
Nilipomaliza na mtumishi Farouk nikamgeukia ndg. mwingine aliekuwa anatushagaa wakati tukiomba na mtumishi Farouk.Huyu ndg anaitwa Komba na anaishi Kibaha mkoani Pwani.Yeye naye nikamweleza kuwa anapaswa kumpa YESU maisha yake.Kwanza aliniambia kuwa yeye hahitaji kuokoka maana yeye ni mkatholiki, nilipomweleza kuwa Biblia inasema kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu ndipo nilipomwona machozi yakimlengalenga na kusema kuwa yupo tayari kumpokea YESU pale pale.....glory to GOD...what a blessing is this...!I tell you it was fantastic....
Naye nikamwongoza sala ya toba na baada ya muda mfupi akawa ameokoka.
Natazamia kwenda Kibaha kesho kumtembelea mtumishi Komba na leo nitamtembelea mtumishi farouk ili nimpeleke mahali pa kuabudu hasa ikizingatiwa kuwa yeye alikuwa muislam kwa hiyo hata kanisani kwake ni msamiati mkubwa.
Naomba wana sayuni popote popote pale mlipo duniani muwaombee wapendwa hawa ili Mungu awatie nguvu waweza kuendelea na wokovu.
Nitaendelea kuwaletea shuhuda za matendo makuu Mungu anayofanya pale Bwana anaponipa kibali.

4 comments:

Anonymous said...

HALELUYAH!!! MUNGU APEWE SIFA.Mtade your doing things which most of born again christian are not doing any more.

Mungu akupe nguvuv tena na tena

Anonymous said...

Hallo Mtade,,

HOngera kwa kazi ya Bwana uliyoifanya hapo kwenu kariakoo.Mungu wetu yupo tayari kumtumia mtu yeyote anapokuwa tayari kutumika.Naamini Mungu anakuandaa kwa utumishi hivi karibuni,mavuno ni mengi, watenda kazi ni wachache.Naungana nawe kuwaombea Farouk na Komba ili wasonge mbele katika maamuzi waliyoyafanya,, Kwako Mtade, wewe sasa ndio mchungaji wao, kwani umewaonesha njia ya kuendea, hivyo uwe nao karibu kwa neno na ushauri mbalimbali wa kiroho.God bleesss you and keep up the servantship spirit in you!
Sauti ya nyika.

savedlema said...

Mtade Bwana Yesu asifiwe sana!
Unajua nimesoma testimony hii hapa nimebaki natabasamu utafikiri mimi ndiyo Yesu, sipati picha yeye anafanyaje huko juu alipokaa na BABA yetu?
Tatizo wapendwa tumezidisha aibu mbaya,yaani tena kwa mwislam ndiyo kabisaa!
What you have done Mtade kinanitia moyo sana,Imefikia mahali wapendwa tuwe kama askari mwamvuli, tukikaa kwenye gari, tukiwa masomoni, kila mahali tupatapo mwanya ni HABARI NJEMA ZA YESU.
Hebu oneni watumishi wa adui yetu wasivyo na haya..wanajua kabisa umeokoka tena huwa unahubiri lakini wakikaa na wewe wanakuachia mapaja wazi..
Shime walokole wenzangu tuianze kazi!
Mtade, nakutia moyo, umeanza na furaha moyoni mwako, sometimes kuna mambo ya kukatisha tamaa, yakitokea usikae kimya.
Love,
Lema

Anonymous said...

Nashukuru sana watumishi wa Mungu Sauti ya Nyika,Savedlema,Kalenge,Maranatha na wengine kwa kunitia moyo katika utumishi huu wa kumletea Bwana mavuno.Nimetiwa moyo sana.
Tuendelee kumtumikia Bwana maadamu ni mchana ...maana usiku unakuja asipoweza mtu kufanya kazi...
Mbarikiwe...
Mtade