Friday, April 18, 2008

TUJIKUMBUSHE-1

Mji wa Nazareti ukionekana hapo juu,mt 2:23, watu wengi walikuwa wakulima, Yesu na Josefu walikuwa maseremala, hivyo ilikuwa rahisi kufahamika. Jangwa la Yudea, linatukumbusha safari ya waisrael, Kujaribiwa kwa Yesu na maisha ya Yohana kuna wakati alikaa Jangwani.
MEGIDO,Armageddoni mahali ambapo vita ya mwisho itapiganwa, this is real, bible haijaficha kitu.
Hili si kaburi la YESU bali ni mfano wa kaburi la Yesu hata sasa yapo

Mfano wa mti aliopanda Zakayo wakati anataka kumwona Yesu ''live'' Yesu lipoingia nyumbani mwa Zakayo akasema ''wokovu umeingia nyumbani mwa Zakayo''

CLICK PICHA UANGALIE KWA UZURI ZAIDI
Be blessed

Kalenge

3 comments:

Maranatha said...

Hahahahaha! Hii picha ya mwisho imenifurahisha sana. Kuna jamaa wako mtini (ila wao sio wafupi kama Zakayo)wakiigiza alivyofanya Zakayo. Ila tuache mambo yote aliyofanya Zakayo yahitaji moyo mkuu. Jamaa alikuwa tajiri na mtu wa heshima. Kisha kwenda kupanda mti?? Nani leo kingunge wa chama na serikali anaweza acha kukalia Masofa yake ofisini penye AC na kwenda kushiriki ibada kwenye mabenchi yasiyo hata na sponji? Ni nani leo yuko tayari kushuka ili Bwana amtumie? Hakika ni wachache. Ahsante Zakayo kwa kutupa somo kubwa. Kwani ulidharau fahari yako na heshima yako kwa ajili ya Kristo na leo hii jina lako limetajwa katika Biblia, naamini pia limo katika kitabu cha uzima, mbinguni.

Shime wapendwa hatuwezi ongeza majina yetu kwenye biblia, lakini mbinguni kwenye kitabu cha uzima,RUKSA!, na tugangamale kwa kumshikilia huyu YESU na kuidharau aibu hata tushiriki nae kwenye ile karamu ya mwana kondoo!

NEVER PLAN TO MISS THE EVENT, I WLL BE THERE TO CELEBRATE WITH JESUS!!! Amen!!!

imanimartini2222 said...

Amen Maranatha , tuombeane mpendwa that place, HEAVEN is not the place to miss.

Lazarus Mbilinyi said...

Maranatha,
Umenikumbusha mbali sana hizo habari za Bwana Zakayo. Ni kweli alikuwa mtu tajiri na mwenye mali, ila alizipata kifisadi ila kitu kimoja alipokutana na Yesu alibadilika, sasa tuje kwetu, je kuna siku viongozi wetu mafisadi wanaweza kujitokeza na kupanda kwenye mti wamuone Yesu? na kufanya yale Zakayo alifanya? hela wanazowaibia watanzania na kuwarudishia na kuwapa mara nne zaidi, maana zina riba. Naipenda sana hiyo habari ya Zakayo huyu jamaa anatakiwa awe mfano kwa viongozi wetu.