Friday, April 4, 2008

Hoja nzito ---Shuhuda za misukule

Hii ni hoja ambayo imeletwa hapa na mdau wa mlima sayuni.Japo hajajitambulisha anaitwa nani na anatokea nchi gani lakini tumeona kuwa hoja zake ni zenye nguvu na yakini.Hebu soma hapa:

Mtumishi,shetani huwa anafanya hivyo, anakupeleka mahali fulani kwa mbwembwe halafu anakuacha.Biblia imeonya mara nyingi msimpe nafasi shetani, huwa hafanyi makosa akipewa nafasi, anaharibu, anaua na anachinja.Hainiingii akilini kama jambo la misukule au wachawi kukamatwa ni jambo la kuutangazia ulimwengu, hata wasio amini. Hiki ni chakula kigumu kwao na wengi huwa hawaelewi badala yake huishia kuona kuwa kumbe ukristo kuna uchawi!!! hawajui.Hata Yesu alipoponya kuna watu aliwaambia msiseme. kuna mahali walimwambia anatumia nguvu za giza!! maana hawaelewi.Kuna shuhuda za kutangaza kwa watu, na zingine tunazimeza kwanza, lengo ni kuwa hawa watu wanaodondoka kwa uweza wa Mungu, ndio wa kwanza kwenda kueleza wachawi wenzao kuwa Yesu, anaweza, ushuhuda!!Tukitaka sifa za kuleta watu na kuwajaza makanisani matokeo yake ni aibu kama hizi.WATU HAWAONGOZWI TENA KWA ROHO, WANAONGOZWA KWA UTASHI WAO, WAMEMZIMISHA ROHO MTAKATIFU.KINACHOBAKI NI AIBU.KUNA vyakula vya kuwapa watu wanaomjua Yesu na vingine havieleweki kwa wasiomjua, tunaposema kutangaza ukuu wa Mungu sawa, lakini mpaka Roho akuambie asiposema kaa kimya.Roho ni msaidizi, Rafiki, Mwombezi,mkumbushaji, mwonyaji, hana papara, huwa anazungumza kwa Sauti ya upole sana,HAAIBISHI usipimsikiliza anakaa pembeni.Huu ni ujinga wetu wenyewe, shetani hana lolote, wala nguvu zake haziwezi kutushinda, ila tumeonywa tusimpe nafasi.Tunajifanya tunajua, Na kipimo ni kuwa WATU WANGAPI WALIOKOKA KWA KUSIKILIZA KUWA WATOTO WAWILI WAMENASWA NA NGUVU ZA MUNGU, KAMA HAKUNA ALIYEOKOKA, HUO HAUKUWA USHUHUDA WA MUNGU.INJILI KUBWA NI SISI KUWA BARUA, NI INJILI YA NGUVU KULIKO HATA MIUJIZA.WALOKOLE TUMEKOSA USHUHUDA WA KUWAFANYA WATU WAOKOKE.Tumewaachia kazi hii wasanii wachache ambao wako tayari kuwaita watu wafanye matamasha ya kuwaenzi wafu. HALAFU WALOKOLE KIBAO WANAENDA,.BILA MAANADIKO NA MAARIFA YA MUNGU, TUTAANGAMIA, TUTAAIBIKA KILA SIKU.NAMALIZA KUSEMA KUWA ROHO HUWA ANAMUANDAA MTU FULANI AOKOKE KWA NAMNA FULANI, KAMA AKIKUAMBIA USHUHUDA HUU SEMA LAZIMA KUNA MTU UTAMLENGA AMA SIVYO NI KUPOTEZA MUDA NA KUTAKA SIFA.NINA WASIWASI WACHUNGAJI WENGI WA SASA YESU AKIRUDI GHAFLA WANAWEZA KUUA TENA!! maana hawafanyi bliblical things.KUNA WACHUNGAJI NASIKIA WAMEANZA KUWEKA PICHA ZAO KUTANGAZA MAKANISA !!!! KILA MCHUNGAJI AKIWEKA , NCHI NZIMA ITAJAA PICHA ZA WATU.YESU ATUSAIDIE.mwanadamu akitaka kuhalalisha kitu hata kosa sababu wala pengine andiko.

1 comment:

Kalenge said...

Kaka Mtade ni mimi Imani nilituma ujumbe, huo, niliandika haraka , nashukuru kuwa ni msaada.Mungu atupe nguvu