Saturday, April 19, 2008

WAKINA DADA KATIKA HUDUMA

Wakina dada katika Huduma;
Bwana Yesu apewe sifa!!
Siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakazi wa jiji la Arusha walishuhudia jambo la kihistoria na la kutia moyo katika shamba hili la Bwana tulilopewa kulilinda.
Ni siku ambayo mwandishi wa Sayuni alishuhudia dada mmoja akihubiri Neno la Mungu katikati ya Jiji hili la Arusha, tena pembezoni wa barabara kuu ya Moshi-Arusha na ile iendayo Nairobi. Dada huyu aitwaye Tunu ambaye anonyesha kuwa ni mkenya, ni dada ambaye kiumri bado ni mdogo ukilinganisha na watumishi wengine wenye ujasiri kama huo. Mwandishi wa blog hii alimshuhudia akihubiri habari za Yesu kwa uwazi kabisa karibu na kituo cha Florida hapa Arusha. Watu waliponywa na kufunguliwa kutoka katika vifungo vya giza. Watu wengi walikusanyika kumsikiliza dada huyu, hata kama vijana wa mjini baadhi yao walipuuzia na kukebehi, yeye hakujali, alifanya alichotumwa na Bwana Yesu. Mwandishi wa blog hii aliiona huduma ya dada huyu akiwa kwenye gari lakini alijisikia kushuka na kurudi kubarikiwa na huduma ya dada huyu.
Inaonyesha kuwa mtumishi huyu alialikwa kutoka Kenya na kanisa moja la hapa Arusha.
Jamani kina dada na wakina kaka wa hapa kwetu Tanzania, tupo wapi? Tupo wapi mpaka dada huyu ameitwa kutoka Kenya kuja kulisha shamba la Bwana hapa na sisi tunaangalia tuu? Tumewaachia kina-Mwakasege na wengineo mpaka kimezidi! Tunategea kwa kweli. Mimi nimetiwa moyo sana na ninawatia moyo vijana wenzangu, tukaze viuno vyetu, tukaifanye kazi ya Bwana.
“Yesu akamuuliza, Simon Petro, je wanipenda?.....akamwambia,”LISHA KONDOO ZANGU”

Mungu aketiye mahali pa juu awajaze nguvu kwa kusudi lake.
www.lema.or.tz

1 comment:

Anonymous said...

Hello. This post is likeable, and your blog is very interesting, congratulations :-). I will add in my blogroll =). If possible gives a last there on my blog, it is about the Livros e Revistas, I hope you enjoy. The address is http://livros-e-revistas.blogspot.com. A hug.